Ulipo bei ya dagaa sh ngapi?

Ulipo bei ya dagaa sh ngapi?

Yohimbe bark

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2019
Posts
2,160
Reaction score
5,728
Habari wakuu,

Kwa wale wapambanaji wenye interest na biashara ya dagaa tunaweza kufanya biashara mimi sasa nipo kisiwa cha GOZIBA bei ya dagaa kwa sasa kwa gunia la dumu kumi ni 180000 mpaka 190000 leo zilifika mpaka 200k kwa gunia.

Dagaa ni nzuri sana sasa hivi mimi nauzia mwanza, kwa wale mlioko mikoani, Mbeya, Arusha, Morogoro, Kigoma, Dar es Salaam na Wilaya za Bariadi, Silali na Kahama huko bei zikoje? kama zinalipa tufanye biashara.
 
Hapo mwanza unauza kwa bei gani?
Mwanza soko sio zuri sana sasa hivi ni 220k mpaka 230k hapo unapata kwa shidi huku visiwani wafanyabiashara wengi hawauzii mwanza wanapeleka mikoa mbali mbali ila sasa kukupa connection ni issue
 
Dah!! Dagaa, usinikumbushe. 🤣😂

Nacheka kama mazuri ila inasikitisha.

Siku moja katika harakati zangu, nilikuwa naenda nje ya mji kidogo(shamba)
Nikafika center kuchukua mazaga zaga, nikakuta maza mmoja(mshua saana, kuanzia ngozi, na kila kitu) alikuwa na mtoto mdogo,
Wakati naendelea kuchukua zaga zaga pale...
Muuzaji alikuwa anakula ugali dagaa, si ndio yule dogo kuropoka..
"Mama muone huyu anakula chakula cha mbwa"
.. dah! Nilijisikia fedheha as if mimi ndio muuza genge.
Bimkubwa akajidai kumpotezea mtoto ndio kamganda mama yake anamtikisa, mama muone huyu anakula chakula cha mbwa..
Bimkubwa ikabidi aombe radhi pale.
 
Kilitokea nini mkuu?

Back
Top Bottom