Dah!! Dagaa, usinikumbushe. 🤣😂
Nacheka kama mazuri ila inasikitisha.
Siku moja katika harakati zangu, nilikuwa naenda nje ya mji kidogo(shamba)
Nikafika center kuchukua mazaga zaga, nikakuta maza mmoja(mshua saana, kuanzia ngozi, na kila kitu) alikuwa na mtoto mdogo,
Wakati naendelea kuchukua zaga zaga pale...
Muuzaji alikuwa anakula ugali dagaa, si ndio yule dogo kuropoka..
"Mama muone huyu anakula chakula cha mbwa"
.. dah! Nilijisikia fedheha as if mimi ndio muuza genge.
Bimkubwa akajidai kumpotezea mtoto ndio kamganda mama yake anamtikisa, mama muone huyu anakula chakula cha mbwa..
Bimkubwa ikabidi aombe radhi pale.