Jitu la-Mtumba
JF-Expert Member
- Mar 20, 2025
- 283
- 760
Habari za wekeend wanajukwaa. Hongereni kwa ibada wanaoenda siku kama ya leo,naamini wengine wameenda juzi na jana ila wote tunamuomba Mungu mmoja wa haki. Hakuna anayeenda ibada kuombea maovu,hata mizimu nayo huwa inaombwa mema.
Octoba 29 tntk! Utachagua mwenyewe irabu za kujaza hapo ila changia maada.
Bwana mimi nielezee kwa ufupi tu upokeo wa rafiki zangu pale nlipofungua biashara yangu.
Nlikuwa na rafiki yangu wa karibu sana tulikuwa tunapanga mipango ya kujikwamua muda mrefu,kupeana mbinu za hapa na pale,mimi nikiwa mkoani wanaita kijiji kikubwa hapa kusini yeye yupo Mwanza.
Kuna kazi akawa anafanya huku kusini,mara ya kwanza anafika hakuwa na wenyeji- akafika kwangu,nikampa full support ya malazi,usafiri sababu hakuwa na wenyeji nampeleka vijiji vya karibu kukutana na watu wake bure kabisa kwa siku zote mpaka anamaliza issue zake anarudi zake,nilikuwa naua ratiba zangu zote sababu napenda kijana mwenzangu akifanikiwa! yule rafiki yangu alikuwa anashukuru saaana sana,
Tumefanya hivyo zaidi ya miaka mi 3 kwa style ile ile,mara mwisho alikuja nimeshakuwa na familia na ofcourse sikuwepo hapa mkoani nikawa nimeingia mjini kimajukumu,kwa kuwa ni mtu wangu wa karibu- nikamtafutia usafiri wa kumzungusha kwenye mishe zake na sehemu ya kulala lodge itayomfaa,hii nayo tumefanya zaidi ya miaka miwili baada ya kuoa. Kuna mtu nlimpa hiyo kazi ya kumzungusha vijiji vya mbali hapa,sometimes wilayani!mara ya mwisho huyo jamaa akaja niambia huyo jamaa yako siyo mzuri! Kwa kweli sikumuelewa!
Point ni pale,nlikuja kumshitukiza kuwa nafungua biashara fulani,ofcourse ikawa ghafla sana kwake na ikatokea. Sasa kwenye ile biashara,wale wateja wake walikuwa wanaweza kabisa kuwa wateja wangu bila kuingiliana katika kazi zake! Mfano:- yeye ananunua mahindi,mimi nawauzia mbolea,na wala sina mpango wa kuja kununua mahindi ko hatutaingiliana kwenye biashara yake [ huu ni mfano]
Yule rafiki yangu nlimuomba namba tu,niweze kuwapa taarifa wateja kuwa kuna kitu fulani unaweza kipata hapa hapa mbeya.
Yule rafiki yangu alikataa kabisa katu katu! Akasema wewe tafuta watu wako wapya,uta enjoy hawa hawata furahia,naanzaje kwanza?! Nlishangaa sema nikachukulia kawaida.
Hadi sasahivi bado huwa nawaza yule msukuma kwanini alikuwa hivyo! Nlikuja kwenda Mwanza kuchukua mzigo,jamaa ushirikiano ulikuwa sifuri,namwambia kitu fulani naweza pata wapi,watu anawajua ila anasema ingia mtandaoni uwacheki! Ila yule msukuma!🚮🚮
Mimi sina chuki naye hata hivyo bado naishi naye kinafiki. Nina ushuhuda kadhaa za reactions za marafiki ambazo nlikuwa siziamini kabla, nitakuwa nashusha moja moja kwenye huu uzi
Wewe ushawahi yapitia yapi toka kwa marafiki au ndugu kwenye mishe mishe zako za kujikwamua?