Ulipokeaje na ulikuwa wapi siku ya tarehe 17 Machi, kifo cha Dkt. Magufuli

Ulipokeaje na ulikuwa wapi siku ya tarehe 17 Machi, kifo cha Dkt. Magufuli

Boeing787-8

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2018
Posts
1,155
Reaction score
1,209
Ile siku sitaisahau, nakumbuka since tarehe 06/03,ulizuka uzushi mkubwa uko jamuhuri ya Tweeter kuhusu afya ya Magufuli.

Basi siku ya tarehe 17, nkatoka jobs, SAA nne usiku nkalala,. Wakati nimelala nilisikia simu inaita Ila kutokana na wenge la usingizi sikuipokea,, baada ya dakika 10, nilipigiwa Tena simu,, na mshikaji wangu mmoja, namnukuu " oya jamaa Meko amefariki"

Ukweli sikumpenda Magufuli Ila nilishtuka hatari, Basi muda huo kuingia Tweeter, nakuta ni sherehe kwa baadhi ya wadau wa Tweeter.

msiba ukinikuta Niko Arusha, nimelala.

Vipi wewe mdau ulipataje habari za msiba huu, na ulikuwa wapi.
 
Mie nilikua kitandani najiandaa nilale nikapigiwa simu na sister angu ananiuliza kuna habari gani huko mjini nikamwambia huku shwari hakuna shari akasema mbona nasikia Rais amefariki?

Nikacheka sana nikamtoa wasi wasi sister atulie tulii kuna wazushi wanapenda kuzusha mambo akasema ameona kwa Zamaradi kapost, nikashtuka kidogo nikamwambia wait nitamcall back.

Mie mbio mbio hadi Jamii Forum nakutana na TANZIA kuuuuubwa, nililia kwa uchungu daaaah hadi leo hua napata ukakasi sana kumuita Hayati Magufuli nahisi bado yupo nasi,

Continue to rest easy Mzalendo wa kweli,

[emoji24][emoji24]
 
Huwa nachelewa kulala lkn siku iyo sijui ilikuwaje nikalala mapema, na huwa nalala wasafi fm ikiwa on maana napendaga kusikiliza miziki sana...

Basi imefika saa tisa usiku nikastuka usingizini, ila nikashangaa wasafi fm wanapiga ule wimbo wa "tukutane paradisoo, tukutane paradisoo", nikajua hapa kimenuka.

Kuingia twitter nikakuta wananzengo wamelipuka mnoo kwa furaha+majonzi.
 
Uzuri sikuhio nililala mapema, baada ya kuumwa kutwa nzima hoi hoi...

Nilikuja kuambiwa saa11 alfajiri moyo wangu ulipasuka,sikua na amani kutwa nzima kwa mara ya kwanza niliuona msiba unavyoumaga kwakweli ilikua ni gafla mno mpaka leo nashindwa kuamini. [emoji22]
 
Mimi nilikuwa porini nalina asali na kutafuta dawa za mitishamba.

Usiku tumelala huko huko porini kuna dogo mwenzetu mmoja alikuwa na radio usiku tumelala akafungua kiredio chake akapata taarifa ya huo msiba akaniamsha kunijulisha sikushituka chochote nikarudi kulala kutokana na uchovu wa kutembea toka asubuhi porini.

Kesho yake nimetafuta network nikampigia jamaa mmoja kuconfirm kama ni kweli akasema ni kweli basi kilichoendelea sijui maana sikufuatilia tena habari hizo toka Samia aapishwe.
 
Nilikuwa Dodoma saa kumi alfajir najiandaa na swala ya alfaji napitapita huko twitter hee naona wadau wanafuraha sana.

Japo two weaks before huko twitter na JF wadau waliripoti meko akiwa mahututi nairobi hospital mara kapewa referal india,mara ujerumani

One weaks before wadau wa JF na twitter wakawa wanasema meko kafa.

Hata hivyo sikustuka sana,niliona ni jambo la kawaida sana.
 
Mimi nilikua nimelala, ile nashtuka tu nachujua simu nakutana na msg ya jamaa "Magu kafa mwamba"

Kidogo tu simu inapigwa nkiambiwa niweke TBC1 kuna habari isio ya kawaida.
 
Nikiwa hapa mji dsmlamu nilikiwanakaribia. Kulala bas Niko na jirani angu Apo katuliaa getoni kwake tuli bass jamaaa akakimbia chumbani kwangu kuwa meko amefariki duh nikasikitika snaa.

Kweli nikasema wamemuaa itakuwa Jamaaa alinishangaa sna kwa jinsi nilivyoupokeee msiba huo nilidondosha Choz kbsa nikajikaza kimya kimya bas jamaa aalinishanga sana jins nilivyo upokea alizani nitafuraia ilaa uliniumma snaa ckupenda kifo chake kwa kweli
 
Daah kabla ya tarehe 17 tarehe 9 majaliwa anaenda njombe tarehe 12samia ana ziara tanga siku tatu kabla ya hizo tarehe malaika alikua akizungumza na mimi katika roho.

Nilimuota magufuli mara tatu ni baaada ya kuhutubia mbezi pale alinionyesha mungu magufuli amekufa nilipatwa na roho ya kuomba na kujinyenyekeza mbele za bwana kitu ninacho amini magufuli alikufa tarehe 8 mwezi wa tatu.

Nilimpenda huyu mtu kwa mara ya kwanza namuona magufuli nilikua nampelekea demu wangu zawadi katika siku yake ya kuzaliwa alikua anasoma baobab girls bahati mbaya siku ile ilinyesha mvua daraja la ruvu chini lilikatika mawasiliano ya barabara kutoka msata kuja dar kupitia bagamoyo road hayakuwa yanapitika.

ndipo mwamba alipofika na kurekebisha hali nikamuona niliwaza moyoni huyu anafaa kuwa raisi wa nchi na kweli ikawa nilimpenda sana huyu mwamba toka moyoni sijipiga kura tena nilianza kwake utamadun wa kupiga kura na umeishia kwake kibaya na kinachoniuma demu niliyempenda kaniacha na mwamba amelala milele ninamaumivu two side ni hayo
 
Nikikuwa nakula monde tartiibu mida hiyo akanipigia patna wng..

Vipi upo wapi??alikuwa na raha sana!!
Nikamjibu chuga hapa njiro contena!!

Akaniambia usiondoke hapo but agizia nyama na bia nakuja!!

Alikuwa anatokea boma(hai)!
kweli alifika na mimi sikuwa na taarifa yoyote pamoja na kuwa nilikuwa bar!

Amefika akiwa na raha sana.
Vipi man umeotea korongo nini??!!
aaahh wapi mwana si magu kanyooka mzeiya!!yaani nimekuja huku tukae leo tule bata adi monii...

Daahh ndo nikajua ila nikachkulia poa tu.
 
Back
Top Bottom