Ulipokeaje na ulikuwa wapi siku ya tarehe 17 Machi, kifo cha Dkt. Magufuli

Me nilikuwa v lounge, moshi town, nakula vyombo na mchuchu, sina hili wala lile, mara simu inaita, na mziki, nikasema bro ni nn usiku usiku na misimu.

Yaye hakuwa anamkubali Magu, mimi namkubali mbayaa, hadi kiama. Zile fununu tukawa tunabishana sana wanamzushia. Napokea simu naziba sikio moja nimsikilize freshi.

Bro ananiambia, dogo cheki tbc Samia anahutubia taifa, nilivosikia tu hivyo, moyo ukapiga paaa.
 
Nipo Mkoani Tanga Lushoto huko nacheki Game ya Uefa Chelsea vs A.Madrid sina hili wa lile kuna jamaa akaropoka Magufuli kafariki..watu fasta fasta wakaingia kwenye simu zao kuverify..aisee mpira haukutazamwa tena.
 
Nilikuwa nyumbani.Ilikuwa ndiyo siku pekee katika maisha yangu ambayo niliwahi kuwa na furahaa kupitiliza.

Nakumbuka kwa mara ya kwanza katika maisha yangu siku hiyo nilitoa sadaka ya kuteketeza kumshukuru Mungu kwa kuniondolea uchafu katika Taifa langu.
 
Nilizipata alfajiri ya tarehe 18, muda ambao Samia alitangaza nilikuwa nimelala zangu fofofo
 
Hiyo siku nakumbuka nilikuwa natoka Mbeya,tupo kwenye coaster,muda wa saa tano hv usiku,tulikuwa mafinga,abilia wote wanasinzia, mmoja akacheki mtandaoni,akasema Jiwe kafa, watu wakashituka, usingizi ukaisha, story zikaanza hakuna aliyelala mpaka tunafika Morogoro, watu walikuwa kama wametoka kifungoni, Jiwe alikuwa shetani
 
Nilikuwa nimelala one of my sons akaja nigongea dirishani kunijulisha kuwa Mheshimiwa ni kweli ameondoka.

Habari zilikuwa zimeshaenea japo hazikuwa rasmi.

Japo Magufuli (Rest well ) aliniumiza sana mahali mahali ila sikupenda alivyokufa kirahisi kuliko hata raia wa kawaida.

Anyway hayupo tena.
 
Ilikuwa usiku, nikasikia Tanzia. Kifupi kwanza si kulala hadi asubuhi, na hamna msiba niliowahi kutoa machozi kama wa hayati Magufuli. Mimi ni mmoja wa watanzania tulioumia sana na kufariki kwake. R. I. P Magufuli
 
Nililala na mipombe sema niliposhtuka usiku wa manane nikaingia jf kama ilivyo kawaida ndipo nikaona TANZIA.

Huwezi amini usiku uleule nililewa zaidi maana kuna jirani nilimpa taarifa akaamka tukamgongea mangi tukaanza kulewa upya.... Mangi mwenyewe alilewa hatari mpaka asubuhi.

Ilikuwa pati la kimyakimya
 
Nilikua safarini nimelala lodge na chui zilikua kichwani nimekuja kujua asubuh kumekucha.
 
Pole mwanamageuzi mwenzangu mwamba kaanguka wanafiki ndo tunawaona sasa so sad ishi nao ila usiwaamini (wanadamu hao)
 
Aisee nakumbuka hii siku nilikuwa nipo room na mtoto wa kike namnyoosha baada ya goal 3 kwenda nyavuni tupo bed tumepumzika ndio nachukua cm naona kila mtu anapost, i was ooh shit kumbe kigogo alikuwa anasema by the way sikuwa shocked sana maana yule bwana kule twitter alikuwa anatupa newz za nini kinaendelea baada ya meko kutokuonekana siku kadhaa
 
So mzigo uli cancel kula au show ngumu
 
Hivi kifo chake hakikutangazwa kwanza na makamu wake? I mean watu walianza kupata habari kabla Samia hajatangaza? NB: Sizungumzii ule uvumi uliokuwepo tangu aanze kuugua mpaka kwenye tarehe 12 Chahali alipoandika rasmi kwenye Twitter kuwa amekufa. Naulizia serikali kutangaza rasmi. Turudi kwenye mada: Mimi niliposikia ni mgonjwa nilikuwa na mashaka kwani kile kipindi kingine alivumishwa tena anaumwa taabani.

Kengele ya tahadhari ilianza kulia siku gazeti la Daily Nation lilipoandika kuna kiongozi kalazwa Nairobi Hospital. Nilijua hili gazeti hawakurupiki lakini cha ajabu kesho yake wakaandika tena hakuna kiongozi aliyelazwa. Baade nikapata habari kutoka chanzo cha kuaminika kuwa ni kweli amepata corona ila hali yake haijulikani. Siku mama Samia alipoenda Tanga na kusema kuchekiwa chekiwa ni kawaida kwa binadamu nilijua lazima kuna jambo ila nikasema huenda ame-recover.

Nilijua rasmi alfajiri baada ya taarifa kutolewa usiku. Na hili la kutangaza usiku lilikuwa ni timing kwani walikuwa hawataki habari itoke mchana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…