Ulipokua Sunday school pambio gani unakumbuka?

Ulipokua Sunday school pambio gani unakumbuka?

Nimekumbuka mwingine....
Upendo wa Mungu ni mkuuuu
Unapita vitu vyoteeee
Hata milima mirefuuuu

sijui nini na nini........
......
Kwa kuandika Upendo huooo wino unge ee kwishaa.

bahari na ziwe winoo mbingu ziwe karatasi na miti iwe kalamu kila mtu awe mwandishi kulihusu Pendo hilo wino ungeee Kwishaa. wimbo mzuri sana huu naupenda mpaka kesho
 
Halafu huu wimbo lazima kuwe na viherehere wawili yaani anaeseeema
Miiiiiiiiiileleeeee
Na kundi la masela wanaitikia
Daimaaaaaaaaaa
Yaaani unaitikia mpaka unasikia koo linataka kung'oka
Hahaha umetisha mzee.
 
Heri wenye moyo safiiii heriii x2
Maana watamwona bwana heri

Kengelee........
Askari wa sunday school
Inapogongwa tunafurahia sana
Asante mwalimu uliyetufundisha
Kwa masomo yetu ya siku ya leo

Dah kitambo xana st. Paul Anglican church Mpwapwa hyo
 
Yesu anapenda watoto x2 Kenya Uganda na Tanzania Yesu anapenda watoto. Nimemkumbuka mwalimu Flora wa Maramba Tanga PAG
 
Back
Top Bottom