Ulipona Ugonjwa wa “Surua” na “Tetekuwanga” kwa dawa za Hospitali au za Asili?

Ulipona Ugonjwa wa “Surua” na “Tetekuwanga” kwa dawa za Hospitali au za Asili?

realMamy

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
3,925
Reaction score
8,853
Inaelezwa kuwa karibu watu wote wanaugua Surua na Tetekuwanga kwa nyakati tofauti katika ukuaji wao.

Mara kadhaa nimeshuhudia wazazi wengi wakiwatibu watoto wao kwa dawa za Asili wakieleza kuwa hutibu haraka na kwa uhakika.

Lakini kwanini hawataki kuwapeleka Hospitalini kupata ushauri wa kitaalamu na kupatiwa dawa sahihi?

Unakumbuka nini kuhusu Surua na Tetekuwanga? Karibu.
 
Dawa sahihi zipi ikiwa umesema wao hueleza kuwa dawa za mitishamba hutibu kwa usahihi na haraka? Kuna ushauri wowote wa maana kuliko kutibu ugonjwa na kupona?

Kuna magonjwa mengi sana hospitali hayatibiki au huchukua muda mrefu kupona kuliko tiba asili.
 
Nakumbuka niliugua Tetekuwanga mwaka 2005 nikaandikiwa dozi ya sindano siku tano mfululizo nikapona. Nilikua kijana machachari sana nikakatwa kwenda shuleni nisije waambukiza wanafunzi wenzangu.
 
Ahahah..kipindi hiko wimbo wa dudubaya unavuma ule video alifanya na yule muigizaji sandra .. mle ndani kuna kipande anaimba "simika mziziz" sandra anajibu "tetementeee"😂😂😂😂
😅😅😅😅😅😅
 
Kuna mti naujua kwa kuuona ila ni mkubwa na utumika kama mbao .majani yake una chemsha afu una ogea ayo maji unapona haraka .atuja wahi tumia dawa za hospitali kwenye hilo
 
Kuna mti naujua kwa kuuona ila ni mkubwa na utumika kama mbao .majani yake una chemsha afu una ogea ayo maji unapona haraka .atuja wahi tumia dawa za hospitali kwenye hilo
Nguvu ya Dawa za Asili 👏🏻
 
Inaelezwa kuwa karibu watu wote wanaugua Surua na Tetekuwanga kwa nyakati tofauti katika ukuaji wao.

Mara kadhaa nimeshuhudia wazazi wengi wakiwatibu watoto wao kwa dawa za Asili wakieleza kuwa hutibu haraka na kwa uhakika.

Lakini kwanini hawataki kuwapeleka Hospitalini kupata ushauri wa kitaalamu na kupatiwa dawa sahihi?

Unakumbuka nini kuhusu Surua na Tetekuwanga? Karibu.
Kuoga maji ya mabingomabingo ile miti flani mwembamba ipo kama miwa mixer kupaka unga usoni
 
Back
Top Bottom