Ulisema "kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake!" Una habari Kuna mbuzi wana kamba moja tu!

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
32,529
Reaction score
76,691
Ndio tumekubali tutakula kwa urefu wa kamba zetu,lakini unajua Kuna mbuzi wanakamba moja tu..?

Wewe unakamba nyingi na nyengine wawezakuwa umezisahau ila zipo!.. sikufundishi ila sijui umewawaza wenye kamba moja..?
Kula,kunywa,Kodi,usafiri na gharama zao zote za maisha hutegemea kamba hiyo moja!,vipi Kama kamba hiyo ikisuasua ama kukatika..? Nafikiri unajua nini kitawapata.

Sasa basi jua kuna mtu anakipiga shoti kiti chako! Na ameshikiria waya mkuu ambao waya huo ni nyenzo ama ni kamba ya baadhi ya watu ambao hutegemea Kama kamba yao ya pekee ya kusimama!.
Wanapiga kelele sidhani kama unasikia ila nahakika hata kama husikii basi unaona!.

Vipi na kule kwenye harufu ya fedha umesikia kelele za vijana wakidai pafunguliwe..?
Hili si geni kwako uliligusia kule mwanza wakati wa ufunguzi wa tawi la harufu ya fedha na kauli yako ilisikika hadi kimataifa!,ikaongeza thamani moja kati ya fedha mtandao!.
Lakini bado kupo mahali kunatakiwa pawekwe sawa wao wanajua na kelele zinazidi siku hadi siku... Kwenye hili jua kuna kodi unazozitaka lakini zinakupita kwani watu wako kwenye harufu fedha nahisi wameshiba mi sijui!.

Wenye kamba moja sio kwamba hawaoni,wanaona ila hawana cha kufanya na sio kwamba hawana cha kufanya wanacho siku watakapounga kamba zao na kuongeza kelele ambazo zinaweza pasua ngoma!.

Wafikirie na wenye kamba moja moja maana ndio wengi zaidi na maamuzi yako huwagusa zaidi.
 
Wafikirie na wenye kamba moja moja maana ndio wengi zaidi na maamuzi yako

sizani km ataelewa

FB_IMG_16458812978073491.jpg
 
Baada ya viongozi waandamizi kupewa ruksa ya kula kwa urefu wa kamba, tunatarajia sasa rais atoe tamko la namna wananchi wengine milioni 60 watakavyo survive ikiwa wao hawamo kwenye kundi la walaji wenye kamba.......
 
Hakuna Mbuzi mwenye Kamba Mbili, Ila kuna mbuzi mwenye kamba ndefu sana hivyo anakula eneo kubwa..., yule mwenye kamba fupi atakula eneo dogo, Na asiye na Kamba anao uwezo wa kula hata mtaa wa pili...

Hivyo nadhani labda useme wengine hawajafungwa kamba wakati wengine wananchi tumefungiwa kamba kwenye kokoto hakuna hata majani
 
Tafsiri yangu kamba ni ulaji I mean Kuna watu vipato vyao vinatoka ktk njia moja tu kamba moja!. Ukitafsiri hivyo ulivyotafsiri hautaelewa hata kidogo!.
 
Kuwa na vipato hata mia sio kosa kama ni kwa njia halali, ila kula kwa urefu wa kamba yaani kutumia position yako kwa manufaa yako sio halali wala haifai, hence watunga Sera wahakikishe kuna ajira za kila mtu kupata kipato na watumishi wafanye kazi kwa mshahara wao na sio kutegemea deals kwenye kazi zao
 
Wenye kamba moja ni wananchi, kwenye harufu ya pesa ni B.O. T, lakini pia kodi tunazopoteza kwenye cryptocurrencies mambo ya Bitcoin, forex, vitu kama paypal ni nyingi dunia inakimbia sisi tupo nyuma, akili za viongozi wetu wanazijua wenyewe maana madini, walishauza, gesi waliuza, mbuga hazieleweki, kusimamia hata uvuvi na kujenga viwanda vikubwa vya samaki baharini na kwenye maziwa wameshindwa, hata kujiongeza kubadili mfumo wa elimu ili tupate talent based education na skillfull knowledge bado ni shida, wanalazimisha tuelewe vishazi huru na tegemezi, mkwawa na isike, teknolojia iko mbali sisi bado tuko nyuma sana.
 
Serikali jengeni shule za michezo, tupate wanamichezo mahiri wekeni mitaala bora na muwafundishe kula protini wachezaji wetu wawe na physic bora, jengeni technical school kila kata kwa kuanzia huko fundisheni uchoraji ramani za majengo, usanifu wa umeme, computer ufundi na mambo kadhaa ya computer kama software na programming, ufundi wa umeme, deciration issues hasa za majumba lakini pia decoration za magari watoto wapate ujuzi utawafaa maishani
 
Wenye kamba moja ni wananchi, kwenye harufu ya pesa ni B.O. T, lakini pia kodi tunazopoteza kwenye cryptocurrencies mambo ya Bitcoin, forex, vitu kama paypal ni nyingi dunia inakimbia sisi tupo nyuma, akili za viongozi wetu wanazijua wenyewe maana madini, walishauza, gesi waliuza, mbuga hazieleweki, kusimamia hata uvuvi na kujenga viwanda vikubwa vya samaki baharini na kwenye maziwa wameshindwa, hata kujiongeza kubadili mfumo wa elimu ili tupate talent based education na skillfull knowledge bado ni shida, wanalazimisha tuelewe vishazi huru na tegemezi, mkwawa na isike, teknolojia iko mbali sisi bado tuko nyuma sana.
😀 Unaubongo unaofanya kazi vizuri.
 
Back
Top Bottom