Ulisema "kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake!" Una habari Kuna mbuzi wana kamba moja tu!

Kule walipo na ardhi ya kutosha vijana wa maeneo hayo wafundishwe kilimo biashara na wajengewe vyuo vidogo vya kilimo kwa level yao wapewe mitaji na maeneo walime kisasa kama ni mbogamboga au matunda au mazao mengine kama soya au kahawa walime kisasa, maeneo yenye bahari au maziwa kuwepo na darasa au chuo kidogo vijana wafundishwe uvuvi bora wapewe elimu ya ufugaji hata samaki kwa kutumia cages au mabwawa ya kutengeneza, hao wapewe mitaji kwa makubaliano maalumu ya kurudisha taratibu na watu wahamasishwe pia kutoka nje kupata maarifa mapya
 
Ndio tumekubali tutakula kwa urefu wa kamba zetu,lakini unajua Kuna mbuzi wanakamba moja tu..?

Wewe unakamba nyingi na nyengine wawezakuwa umezisahau ila zipo!.. sikufundishi ila sijui umewawaza wenye kamba moja..?
Kula,kunywa,Kodi,usafiri na gharama zao zote za maisha hutegemea kamba hiyo moja!,vipi Kama kamba hiyo ikisuasua ama kukatika..? Nafikiri unajua nini kitawapata.

Sasa basi jua kuna mtu anakipiga shoti kiti chako! Na ameshikiria waya mkuu ambao waya huo ni nyenzo ama ni kamba ya baadhi ya watu ambao hutegemea Kama kamba yao ya pekee ya kusimama!.
Wanapiga kelele sidhani kama unasikia ila nahakika hata kama husikii basi unaona!.

Vipi na kule kwenye harufu ya fedha umesikia kelele za vijana wakidai pafunguliwe..?
Hili si geni kwako uliligusia kule mwanza wakati wa ufunguzi wa tawi la harufu ya fedha na kauli yako ilisikika hadi kimataifa!,ikaongeza thamani moja kati ya fedha mtandao!.
Lakini bado kupo mahali kunatakiwa pawekwe sawa wao wanajua na kelele zinazidi siku hadi siku... Kwenye hili jua kuna kodi unazozitaka lakini zinakupita kwani watu wako kwenye harufu fedha nahisi wameshiba mi sijui!.

Wenye kamba moja sio kwamba hawaoni,wanaona ila hawana cha kufanya na sio kwamba hawana cha kufanya wanacho siku watakapounga kamba zao na kuongeza kelele ambazo zinaweza pasua ngoma!.

Wafikirie na wenye kamba moja moja maana ndio wengi zaidi na maamuzi yako huwagusa zaidi.
Rais anashughulika na kuwaongezea kamba zaidi
 
Balozi zetu zitafute masoko ya mazao yetu kwa nguvu zote balozi wa Angola atafute soko la maharage huko liwe la kudumu, balozi wa china aongeze wigo wa uuzaji wa soya lakini pia soko na Nguruwe, aliepo congo atafute soko kubwa la mawese na mbuzi na mchele, kila balozi asiishi kama celebrity apambane kusaka fursa na aje kuelezea umma nini kaipatia nchi yake
 
Baada ya viongozi waandamizi kupewa ruksa ya kula kwa urefu wa kamba, tunatarajia sasa rais atoe tamko la namna wananchi wengine milioni 60 watakavyo survive ikiwa wao hawamo kwenye kundi la walaji wenye kamba.......
Zero brain
 
Kule walipo na ardhi ya kutosha vijana wa maeneo hayo wafundishwe kilimo biashara na wajengewe vyuo vidogo vya kilimo kwa level yao wapewe mitaji na maeneo walime kisasa kama ni mbogamboga au matunda au mazao mengine kama soya au kahawa walime kisasa, maeneo yenye bahari au maziwa kuwepo na darasa au chuo kidogo vijana wafundishwe uvuvi bora wapewe elimu ya ufugaji hata samaki kwa kutumia cages au mabwawa ya kutengeneza, hao wapewe mitaji kwa makubaliano maalumu ya kurudisha taratibu na watu wahamasishwe pia kutoka nje kupata maarifa mapya
Rais analishughulikia hili kwa kuwafikishia barabara na Sasa amesema anaenda kuangalia mfumo wa Kodi kuondoa double taxation
 
[emoji3] Unaubongo unaofanya kazi vizuri.

Mambo ni mengi kuna muda unawaza unaona hawa jamaa nia yao sio kuliinua taifa bali kujiinua wao kiuchumi, halafu issue zenyewe wanatakiwa kufanya ni za kawaida sana lakini mara mchakato, mara utafiti na blah blah East Africa kenya imekua hub ya makampuni makubwa duniani sababu waliipokea teknolojia mapema zaidi, Tanzania iko kwenye best position tena ilipendelewa na Mungu lakini penye miti hakuna wajenzi
 
Tatizo viongozi na system ya uongozi ilishakuwa ya ajabu!
 
Rais analishughulikia hili kwa kuwafikishia barabara na Sasa amesema anaenda kuangalia mfumo wa Kodi kuondoa double taxation

Kama mfumo wa uzalishaji ni stable kodi wananchi tutalipa kwa moyo mmoja maana hata misaada tunayopewa ni kodi za watu wengine huko duniani, lakini pia uwazi kwenye kodi kwa mfano ijulikane kontena ya bidhaa fulani 40ft au 20ft kodi yake kiasi kadhaa mzigo umefika mtu anaenda kulipa kile kiasi anarudi pale na slip naonesha mzigo unakaguliwa anaondoka, haya vibanda vya mtaani hakuna sababu ya kukimbizana waelezwe kila kibanda kwa mwaka ni labda laki moja mtu alipe achape kazi anaenda TRA kufuata control namba tu sio kwenda mara akadiliwe then akiona makadirio makubwa anafunga na kibanda chenyewe anaondoka lazima tubadilike mambo yawe wazi
 
Tatizo viongozi na system ya uongozi ilishakuwa ya ajabu!

Ndio tunabaki tunaokoteza kodi kubwa kwenye nyenzo za usafiri yaani gari used japana, dubai, china, thailand, marekani iko bei chini kosa uweke kodi rafiki wananchi waongize magari kwa wingi ili purchase ya mafuta iwe juu na shughuli ziimarike na kurahisika unapiga kodi kubwa kuliko manunuzi ya gari wakati wewe sio mzalishaji wa gari hiyo tena unaweka formular za wrong calculator ili uumize wananchi, una bandari kila siku unashihudia magari yanapita kwako kwenda nchi nyingine huku raia wako hana uwezo wa kununua gari
 
Weka kodi ya chini sana kwenye magari, na watanzania wahamasishwe kununua na kuuza magari ndani na nje lakini leo car agency za bongo wengi ni madalali wa kuagiza magari ulipe nusu gari ikifika umalizie gharama upewe gari kwa sababu biashara yenyewe iko full stressed na kodi kubwa zisizo na msingi wowote
 
Kama mfumo wa uzalishaji ni stable kodi wananchi tutalipa kwa moyo mmoja maana hata misaada tunayopewa ni kodi za watu wengine huko duniani, lakini pia uwazi kwenye kodi kwa mfano ijulikane kontena ya bidhaa fulani 40ft au 20ft kodi yake kiasi kadhaa mzigo umefika mtu anaenda kulipa kile kiasi anarudi pale na slip naonesha mzigo unakaguliwa anaondoka, haya vibanda vya mtaani hakuna sababu ya kukimbizana waelezwe kila kibanda kwa mwaka ni labda laki moja mtu alipe achape kazi anaenda TRA kufuata control namba tu sio kwenda mara akadiliwe then akiona makadirio makubwa anafunga na kibanda chenyewe anaondoka lazima tubadilike mambo yawe wazi
Stay tuned kwenye bajeti ijayo itajibu changamoto nyingi.Na ikumbukwe ndio bajeti ya kwanza ya Samia,bajeti iliyopita alikuta imepangwa tayari kwa hiyo hangeweza kuwa na intervention San kwa sababu pia ndio kwanza alikuwa anaanza Urais.

As we speak bajeti iko tayari kinachoanza mwezi wa 4 ni kupata idhininya Bunge na michango yao ya boresho tuu.

Mwisho Kodi haichajiwi kwa kontena bali kwa value ya kilichomo kwenye kontena.
 
Ile kucharge kodi kwa kontena ni mfano tu, kwa mfano kuna ubaya gani kontena ya kanga yenye thamani fulani kodi yake ijulikane ni kiasi fulani ili mtu akiagiza anajua hapa itakua hivi nalipa nakupewa mzigo?
 
Kwanza amini bajeti za nchi hii hua hazima vipaumbele vya kueleweka na hua hazitimizwi japo kwa asilimia 50 ingekua utekelezaji wa bajeti zetu ni mzuri tungekua mbali tatizo kwanza bajeti tegemezi wapi uliona ina workout?
 
Ndio tumekubali tutakula kwa urefu wa kamba zetu,lakini unajua Kuna mbuzi wanakamba moja tu..?

Wewe unakamba nyingi na nyengine wawezakuwa umezisahau ila zipo!.. sikufundishi ila sijui umewawaza wenye kamba moja..?
Kula,kunywa,Kodi,usafiri na gharama zao zote za maisha hutegemea kamba hiyo moja!,vipi Kama kamba hiyo ikisuasua ama kukatika..? Nafikiri unajua nini kitawapata.

Sasa basi jua kuna mtu anakipiga shoti kiti chako! Na ameshikiria waya mkuu ambao waya huo ni nyenzo ama ni kamba ya baadhi ya watu ambao hutegemea Kama kamba yao ya pekee ya kusimama!.
Wanapiga kelele sidhani kama unasikia ila nahakika hata kama husikii basi unaona!.

Vipi na kule kwenye harufu ya fedha umesikia kelele za vijana wakidai pafunguliwe..?
Hili si geni kwako uliligusia kule mwanza wakati wa ufunguzi wa tawi la harufu ya fedha na kauli yako ilisikika hadi kimataifa!,ikaongeza thamani moja kati ya fedha mtandao!.
Lakini bado kupo mahali kunatakiwa pawekwe sawa wao wanajua na kelele zinazidi siku hadi siku... Kwenye hili jua kuna kodi unazozitaka lakini zinakupita kwani watu wako kwenye harufu fedha nahisi wameshiba mi sijui!.

Wenye kamba moja sio kwamba hawaoni,wanaona ila hawana cha kufanya na sio kwamba hawana cha kufanya wanacho siku watakapounga kamba zao na kuongeza kelele ambazo zinaweza pasua ngoma!.

Wafikirie na wenye kamba moja moja maana ndio wengi zaidi na maamuzi yako huwagusa zaidi.
Wengine kamba zao ni za mpira, kwa hiyo zinavutika na kufika popote!
 
Back
Top Bottom