Ulishawahi fanya biashara ya kuexport bidhaa nje ya Tanzania?

Ulishawahi fanya biashara ya kuexport bidhaa nje ya Tanzania?

Duh ujipange hiyo biashara sio ya kitoto. Hao kondoo inabidi wawe wamehasiwa ili kuondoa "male odor"/halufu ya kiume/pumbu/korodani ndio wakubaliwe.
Umri na uzito wa kondoo lazima uzingatiwe, vipimo vya magonjwa kabla na baada ya kuchinjwa n.k
Soko lake unalipateje wanao nunua tunawatafuta wap
 
Soko lake unalipateje wanao nunua tunawatafuta wap
Kusema kweli sijawahi ona mtu binafsi ana export nyama nje ila kuna kiwanda cha nyama Kibaha/Soga na Frostan/Mikocheni hawa ndio wana export.
 
miaka mingi kidogo imepita nilifanya kazi kwenye kampuni za usafirishaji mizigo na hasa kwenye idara ya export
najua taratibu zimebadilika sana lakini kwa sasa zinaweza kuwa rahisi zaidi.
nitatoa kila ninachokumbuka kisha wadau watajazia najua wapo hapa.
  1. cha kwanza ni kutafuta mteja na kwa siku hizi ili wal sio tatizo linawezekana
  2. anaweza akakwambia utume sample ya mzigo unaompelekea na hasa kama ni primary product kwa kadri mlivyokubaliana sasa kama ni mazao ya kilimo hapa lazima kitengo cha kilimo kihusike kwa kukuandalia certificate za fumigation ambazo hutolewa na fumigation firm zilizokubaliwa na phytosanitary nimesahau hutolewa na kilimo.
  3. baada ya hapo mnakubaliana terms and condition za kusafirsha mzigo
  4. kama mazao unayosafirisha yana bodi inabidi ulipie 2% ya thamani ya mzigo unaopeleka (zamani)
  5. parking inafanyika kwa kadri ya mteja na document zinatayarishwa
  6. kwenye document nakumbuka kuna
    1. single bill of entry ambayo kwa sasa unajaza na inapita ukiwa mezani
    2. parking list
    3. invoice
    4. na zingine kwa kadri ya uhitaji wa mteja iliajilizishe kuwa mzigo anaonunua ni salama
  7. baada ya kuload mzigo na meli kupakia baada ya muda mchache bill of ladiing inakuwa tayari ambayo unaweza kuambatanisha na invoice na document nyingine kwa mteja kwa ajili ya yeye kukulipa kama alikuwa hajalipa kwanza na kupokea mzigo
  8. miaka ya nyuma kulikuwa hakuna kodi tra zijui kwa sasa
hiki ndicho ninachokumbuka kwa kazi niliyoifanya mwisho 1996
 
Back
Top Bottom