Kama kijana kwenye hatua ya Ujana lazima upoteze mechi moja au kadhaa kadhaa... huwezi shinda zote!
Nilimzimikiaga manzi mmoja kipindi niko elimu ya Juu jijini Dar miaka kadhaa iliyopita chuo fulani nikawa nahudumia vitu fulani fulani mpaka kadogori nilimnunuliaga tena few days baada ya kadogori kake kuzingua na pesa nilichomoa kwenye ada... kale kademu nakumbuka kalikuwa na visa, mideko na mashauzi kama yote ila badae niligundua mwenyewe na kuambiwa kwamba wanawake wa kizanzibar ndo walivyo
Alikula sana Chips mayai zangu, Kuku vidali, sausages na Kachumbari na hata fedha sometimes
Mwisho wa siku akaishiwa kuolewa na mwamba alitutangulia kumaliza masomo mwaka au miaka miwili iliyopita ila niligundua lile kabla hajaolewa na tuliachanaga mapema ila kovu ninalo mpaka kesho...😂
Na bahati nzuri jamaa yake Lofa tu hana hela mjanja mjanja wa mjini hapo ndo nafarijikaga 😂😂😂👍🏾