Ulishawahi kukumbwa na hii hali?

Ulishawahi kukumbwa na hii hali?

lyajody

Senior Member
Joined
Aug 16, 2024
Posts
145
Reaction score
196
Ulishawahi pitia kipindi kigumu hadi ukashindwa kutoa rambirambi za misiba mfano labda una group kama vile watu mliohitimu nao chuo labda itokee msiba mmoja wenu amefariki, unatolewa mkeka wa waliochanga wote wamechanga kasoro wewe tu

Hadi unapigiwa simu kutafutwa unaogopa kupokea na mbaya zaidi sio kwamba unatoa ulichojaliwa kuna kiwango maalumu. Je, ukipitia hali hii unafanya kitu gani?
 
Ulishawahi pitia kipindi kigumu hadi ukashindwa kutoa rambirambi za misiba mfano labda una group kama vile watu mliohitimu nao chuo labda itokee msiba mmoja wenu amefariki...
Unatumia muda na rasilimali zote ulizokua nazo kuinvest kwenye kujitafutia kipato, michango haikufanyi kua na roho nzuri/mtu mwema.

Kitakachofanya uwe na roho nzuri/mtu mwema ni:

1. Matendo mema

2. Kuwa "real"........ni pamoja na kutoa kulingana na kipato chako,mipango yako na bajeti yako
 
Ulishawahi pitia kipindi kigumu hadi ukashindwa kutoa rambirambi za misiba mfano labda una group kama vile watu mliohitimu nao chuo labda itokee msiba mmoja wenu amefariki...unatolewa mkeka wa waliochanga wote wamechanga kasoro ww tu

Had unapigiwa simu kutafutwa unaogopa kupokea na mbaya zaid sio Kwamba unatoa ulichojaliwa Kuna kiwango maalumu..je ukipitia hali hii unafanya kitu gani?
Cha kwanza ni kukubali kuwa wewe ndio Unapitia hali hiyo

Cha pili ni kuwekekeza nguvu nyingi kwenye kuishi MAISHA YAKO na si maisha ya wengine.

Siku zote jilinganishe na wewe mwenyewe ulivokua jana ,leo na jinsi gani utakuwa bora wa kesho.

Tatu ,Ikiwezekana jipe muda kwa kujitoa kwenye magroup ambayo yanakupa presha zisizo na mchango katika kipindi hiki cha kujitafuta ,Unaweza kutumia simu kujiunga na magropu ya fursa za kazi ukawa unatazama zinoendana na sifa zako ukajikit zaidi kwenye kuomba kazi.

Mwisho,Mungu ana nafasi kubwa hasa maombi yako kwake kipindi ambacho una dhiki na uhitaji mkubwa.

Baso
 
Pole sana Mungu akufanyie wepesi
Kwa sasa toa ulichonacho kaa kimya
BTW rambirambi haifufui marehemu
 
Ndio maana mimi binafsi sipo kwenye kundi lolote hata la familia huwa nafanya vyovyote kujitoa.
Inasikitisha sana na kufedhehesha pindi ikikukuta hali hio kwa kweli , na katika situation ya namna hio.
 
Huwa inatokea na inaumiza sana,kifupi huwa ninapokea simu zao, na ninawaambia mimi sina hela this time,sasa atakayechukia aachukie tu, hili ni bora kuliko kwenda kukopa hela huku roho inavuja damu ndani na hata hiyo hela ukitoa inakuwa haina baraka mbele za Mungu, kifupi huwa naangalia amani kwenye moyo wangu...
 
Back
Top Bottom