Utotole
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 6,607
- 4,263
Wakati nakumbana nayo kwa mara ya kwanza ilikuwa mwanzoni-mwanzoni mwa miaka ya tisini. Hesabu yenyewe muulizaji anakusomea kwa njia ya imla (dictation) na wewe unakokotoa. Akimaliza anakuomba umtajie jibu ulilopata. Kumbuka, mkokotoaji anakokotoa kimya kimya.
Na hivi ndivyo inavyokwenda hesabu hiyo.
"Chukua idadi ya wavulana (male siblings) kwenu zidisha mara mbili, jumlisha tatu kisha zidisha mara tano; jumlisha idadi ya wasichana (female siblings), kisha toa kumi na tano"
Jibu utakalompa litamwezesha kujua mmezaliwa wangapi na wavulana ni wangapi na wasichana wangapi.
NB. Kama kuna jinsi mojawapo ina idadi inayozidi tisa, atahitaji kuuliza swali la ziada na kama kuna jinsi ambayo ni sufuri, atauliza pia baada ya kupata jibu maana jibu litaonyesha wazi.
Jaribu uone unapata ngapi. Karibuni.