Ulishawahi kukutana na hesabu kama hii? Tupe experience yako

Ulishawahi kukutana na hesabu kama hii? Tupe experience yako

Utotole

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2010
Posts
6,607
Reaction score
4,263
Wakati nakumbana nayo kwa mara ya kwanza ilikuwa mwanzoni-mwanzoni mwa miaka ya tisini. Hesabu yenyewe muulizaji anakusomea kwa njia ya imla (dictation) na wewe unakokotoa. Akimaliza anakuomba umtajie jibu ulilopata. Kumbuka, mkokotoaji anakokotoa kimya kimya.

Na hivi ndivyo inavyokwenda hesabu hiyo.

"Chukua idadi ya wavulana (male siblings) kwenu zidisha mara mbili, jumlisha tatu kisha zidisha mara tano; jumlisha idadi ya wasichana (female siblings), kisha toa kumi na tano"

Jibu utakalompa litamwezesha kujua mmezaliwa wangapi na wavulana ni wangapi na wasichana wangapi.

NB. Kama kuna jinsi mojawapo ina idadi inayozidi tisa, atahitaji kuuliza swali la ziada na kama kuna jinsi ambayo ni sufuri, atauliza pia baada ya kupata jibu maana jibu litaonyesha wazi.

Jaribu uone unapata ngapi. Karibuni.
 
Utotole yaani umekuwa kama umo kwenye ubongo wangu, hii nilikuwa na mpango wa kufungulia thread, umeniwahi tu.

hapo sasa huwanga naona hesabu kama uchawi, naomba watalamu wa hesabu watufanulie why inakuwa vile, mimi pamoja na kuwa m utafiti wa mambo lakn kwa hapa mimesalenda.
 
Last edited by a moderator:

Shy land, hesabu siyo uchawi, ni kawaida tu kucheza na namba. Ipo nyingine ambayo sasa ndio unaweza kudhani mtu anatumia nguvu za ziada maana mtu anakuambia uandike namba (tarakimu) kwenye karatasi, wewe unaandika labda 7295063. Ukishaandika yeye anaruka mistari kama mitatu chini anapiga msitari kisha anaandika jibu kabisa, na kwa namba hii jibu angeandika 27295061.

Anakupa nafasi uandike nyingine chini ya ile ya mwanzo kisha na yeye anaandika namba, mnaendelea hivyo hivyo kama awamu nne au tano halafu anakwambia uhakikishe kama jibu ni sawa au la. Ukihakikisha jibu unakuta ni sawa bila ubishi.

Na kumbuka kuwa jibu aliliandika mara tu baada ya wewe kuandika tarakimu ya kwanza, na hakukuwa na muda wa kupiga hesabu kila alipotaka kuandika tarakimu zake. Unaifahamu hiyo Shy land? (maana umelianzisha la hesabu za mafumbo leo!).
 
Shy land, hesabu siyo uchawi, ni kawaida tu kucheza na namba. Ipo nyingine ambayo sasa ndio unaweza kudhani mtu anatumia nguvu za ziada maana mtu anakuambia uandike namba (tarakimu) kwenye karatasi, wewe unaandika labda 7295063. Ukishaandika yeye anaruka mistari kama mitatu chini anapiga msitari kisha anaandika jibu kabisa, na kwa namba hii jibu angeandika 27295061. anakupa nafasi uandike nyingine chini ya ile ya mwanzo kisha na yeye anaandika namba, mnaendelea hivyo hivyo kama awamu nne au tano halafu anakwambia uhakikishe kama jibu ni sawa au la. Ukihakikisha jibu unakuta ni sawa bila ubishi.

Na kumbuka kuwa jibu aliliandika mara tu baada ya wewe kuandika tarakimu ya kwanza, na hakukuwa na muda wa kupiga hesabu kila alipotaka kuandika tarakimu zake. Unaifahamu hiyo Shy land? (maana umelianzisha la hesabu za mafumbo leo!)

Ni sawa ni somo la kucheza na mamba lakn kichawi. why 1+1=2
 
Mi mbona hata sijaelewa....jibu la mwisho lina tarakimu mbili af unasema linaonesha idadi yenu,wasichana wangapi na wavulana wangapi...how??
 
Me naifaham mathematics trick ingine mtu anakwambia, Fikiria namba halafu ijumlishe kwa yenyew , halafu atakwambia izidishe kwa namba fulani( anakutajia yoyote kati ya 0-9) halaf atakwambia gawanya kwa namba ulofikiria mwanzo, jibu lake itakua ni ile namba alokwambia uzidishie pale mwanzo, yeye ataizidisha mara 2 io namba ndo jibu lako. Karibuni
 
"Chukua idadi ya wavulana (male siblings) kwenu zidisha mara mbili, jumlisha tatu kisha zidisha mara tano; jumlisha idadi ya wasichana (female siblings), .

ni idadi ya wavulana/wasichana au idadi ya siblings (ndugu wavulana/wasichan)?
 
mbona m napata jbu 20 mkuu emb nambie kwetu tupo wangap?
 
hebu chukulia kuna watoto wawili...mvulana na msichana..

Wakati nakumbana nayo kwa mara ya kwanza ilikuwa mwanzoni-mwanzoni mwa miaka ya tisini. Hesabu yenyewe muulizaji anakusomea kwa njia ya imla (dictation) na wewe unakokotoa. Akimaliza anakuomba umtajie jibu ulilopata. Kumbuka, mkokotoaji anakokotoa kimya kimya.

Na hivi ndivyo inavyokwenda hesabu hiyo.

"Chukua idadi ya wavulana (male siblings) kwenu zidisha mara mbili, jumlisha tatu kisha zidisha mara tano; jumlisha idadi ya wasichana (female siblings), kisha toa kumi na tano"

Jibu utakalompa litamwezesha kujua mmezaliwa wangapi na wavulana ni wangapi na wasichana wangapi.

NB. Kama kuna jinsi mojawapo ina idadi inayozidi tisa, atahitaji kuuliza swali la ziada na kama kuna jinsi ambayo ni sufuri, atauliza pia baada ya kupata jibu maana jibu litaonyesha wazi.

Jaribu uone unapata ngapi. Karibuni.
 
1x2=2
2+3=5
5x5=25
25+1=26
26-15=11

Kwa hiyo 11 ni sawa na ; mvulana mmoja na msichana mmoja. Una swali jingine?

Wewe mkuu Utotole kama uko sawa sawa vile......maana nami nimepita mapito yako nikaona mule mule.

wavulana
4x2=8
8+3=11
11x5=55
55+2=57
wasichana 2
57-15=42

Na ni kweli wavulana tupo 4 na wasichana 2 , sasa sijui ndilo jibu sahihi au nami niko chaka?, wadau mdassa wa kuthibitisha usahihi maaana hesabu malupe lupe tu.
 
Last edited by a moderator:
ni idadi ya wavulana/wasichana au idadi ya siblings (ndugu wavulana/wasichan)?

Vyovyote vile utakavyoamua, hata kama ni ndugu wote na majirani. Mradi jibu nalo liwe concluded hivyo hivyo
 
Wewe mkuu Utotole kama uko sawa sawa vile......maana nami nimepita mapito yako nikaona mule mule.

wavulana
4x2=8
8+3=11
11x5=55
55+2=57
wasichana 2
57-15=42

Na ni kweli wavulana tupo 4 na wasichana 2 , sasa sijui ndilo jibu sahihi au nami niko chaka?, wadau mdassa wa kuthibitisha usahihi maaana hesabu malupe lupe tu.

Uko sawa kabisa
 
Mi mbona hata sijaelewa....jibu la mwisho lina tarakimu mbili af unasema linaonesha idadi yenu,wasichana wangapi na wavulana wangapi...how??

Umepata ngapi? Kama umepata 23 maana yake wavulana mko 2 wasichana 3
 
Me naifaham mathematics trick ingine mtu anakwambia, Fikiria namba halafu ijumlishe kwa yenyew , halafu atakwambia izidishe kwa namba fulani( anakutajia yoyote kati ya 0-9) halaf atakwambia gawanya kwa namba ulofikiria mwanzo, jibu lake itakua ni ile namba alokwambia uzidishie pale mwanzo, yeye ataizidisha mara 2 io namba ndo jibu lako. Karibuni

Hapo trick yake iko kwenye kugawanya kwa namba yenyewe uliyofikiria (unknown)...kwa hiyo inajifuta kwenye equation kimtindo.
 
Kuna kanuni moja anakupitisha ambayo ukiipitia ni kama umemwambia idadi ya siblings.

It's all mathematical.

Ni kama vile nikupigishe mahesabu mengi ya positive number, halafu mwisho nikwambie jibu lake zidisha kwa negative one, halafu nikwambie jibu utakalolipata mwisho ni negative.

Of course ni negative, any positive number times negative nhmber equals negative number.

So wanachofanya ni kuongeza iterations (nyingine hazina mpango, za kukuzingua tu uone process ndefu) halafu wanakunasa na ki process cha kukufanya utoe jibu mwenyewe.
 
Back
Top Bottom