Ulishawahi kukutana na hesabu kama hii? Tupe experience yako

Vyovyote vile utakavyoamua, hata kama ni ndugu wote na majirani. Mradi jibu nalo liwe concluded hivyo hivyo

hujaelewa swali.
sisi tuko watatu. so nasema nina ndugu wawili/two siblings.

so nagesabu Total au Siblings peke yao...?
 
hujaelewa swali.
sisi tuko watatu. so nasema nina ndugu wawili/two siblings.

so nagesabu Total au Siblings peke yao...?

Nimeelewa, wewe ndio hujaelewa maelezo yangu. Namaanisha hivi. Kama ukiamua kupigia mahesabu siblings tu utapata majibu ya siblings. Na kama ukiamua uunganishe na wengine kwenye familia yenu hata kama siyo siblings, utapata jibu pia la jumla. Mfano kama mko watano, ndugu wanne na mwingine labda ni msaidizi wa kazi, ukiambua kupiga mahesabu ya siblings tu tumia wanne, na ukiamnua upige mahesabu ya kila mtu hata baba na mama uweke, utapata pia jibu sahihi. Kinachotakiwa ni kwamba kama idadi uliyoingiza kwenye equation ni ya siblings tu, basi na conclusion i-base kwa siblings tu. Na kama ilikuwa inclusive of everybody, basi ukipata jibu 'kunkulusheni' iwe inclusive.
 
ni kweli ila ni subjective, si lazima iwe ni ndugu zako wasichana na wavulana hata, ukisema majogoo na mitetea, au kimahesabu imekaa hivi 5(2x+3) +y-15=X:Y x=wavulna/jogoo y=wasichana/mitetea
 

Hamna uchawi hapa ilia ni misururu ya ujanja tu. Tayri nishaijua.

Ukitaka vyema, ni vizuri uyaandike yote kwanza:

Fikiria muwe ndugu watatu wa kiume na wanne wa kike. Hivi itakuwa:

(((3 x 2) +3) x 5) + 4 - 15

"Uchawi" uko kwenye zile digits ambazo nimeziweka kwa rangi nyekundu.

Kazi ya "2" ni moja. Unapofungua hizo brackets, 2 itazidishwa na 5 na hii itakupa 10. Hii ten itaazidisha idadi ya ndugu zako mara kumi. Kwa hivyo, kama ndugu wako ni watatu, Idadi hii itakuja 30. Tayari, unaona hapo "3" ndio idadi ya ndungu wa kiume ambayo itajitokeza mwisho wa hesabu.

place value ya ones/units itakuwa free na kuchukuliwa na idadi ya ndugu wa kike. Next ni "3." Kazi ya hii three ni kusafisha "0" yoyote inayoweza kuharibu hesabu. Kwa mfano, je, kama huna Ndugu wa kiume kutakuwaje? Hii ndio kazi ya hii "3".

Kama tulivyosema tayari, Kazi ya five ni fanya "2" iwe "10" na kusongesha idadi ya ndugu wa kiume kuelekea upande wa kushoto na kuacha place value ya wadada iwe "ones." Lakini hii five, ikizidisha "2", pia inazidisha "3" na basi ni lazima itolewe kwani inaongeza hesabu kwa "15". Hii kumi na tano tunaitoa na huu kwa kuondoa 15. kwenye hesabu.

Tatizo na hii hesabu ni kuwa haiwezi kufanya kazi ikiwa una idadi ya ndugu wa kike wanaozidi tisa, kwani place value ya kina dada ipo tu kwenye "ones" na inapozidi 9, basi itakuwa imeingi "tens" na ujanja wake utakuwa umeishi hapo.
 

Uko sahihi. Inakuwa changamoto idadi ya wadad inapokuwa zaidi ya tisa na kama nilivyotoa angalizo, itahiatija swali la ziada ili kupata jibu katika mazingira hayo. Nilichokosea ni kusema jinsi yoyote, maana tatizo hili huathiri hesabu wadada tu wakizidi tisa. Lakini pia inatakiwa kabla ya ku-conclude upate taarifa kama wadada ni zaidi ya tisa, na je, wako katika "tens" au "twenties" au "thirties" idadi yao?. Ikitokea wadada ni zaidi ya tisa, utalazimika kufanya hesabu ndogo tena mwenyewe kabla ya kutoa jibu. Unachofanya ni kuwa ile tarakimu ya kushoto (ambayo kimsingi inawakilisha wakaka) unaivunja kwa kuondoa 1 (in case of tens) au 2 (in case of twenties) kisha kuipachika katikati ya zile tarakimu mbili zilizopatikana kama jibu (ile ya mkumi ikiwa ni baada ya kuondoa ile 1 au 2 or whatever the case may be), then you can make your conclusion. Siku hizi watu wachache wanaweza kuzaa kufikia viwango hivyo...

Mfano 1: Wakaka 5 na wadada 12
5x2=10
10+3=13
13x5=65
65+12=77
77-15=62
(kwa kuwa wadada wako katika makumi, tunavunja 6 kwa kuondoa moja na kuipachika katikati ya 6 na 2 na hapo tunapata 6-1=5
512; 5,12

Mfano 2: Wakaka 6 wadada 24
6x2=12
12+3=15
15x5=75
75+24=99
99-15=84
Kwa kuwa tunajua wadada wako kwenye "twenties" idadi yao, tunatoa 2 toka kwenye 8, thus 8-2=6 na mwishowe tunaandika jibu letu kama 624; 6,24

Hesabu nyingi lazima ziendane na assumptions, lets, given that, na reference to known facts. Kwa hiyo kwa case hii somehow utatakiwa kujua baadhi ya facts in case of unusual situations kama watoto wa kike 21 n.k.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…