Hamna uchawi hapa ilia ni misururu ya ujanja tu. Tayri nishaijua.
Ukitaka vyema, ni vizuri uyaandike yote kwanza:
Fikiria muwe ndugu watatu wa kiume na wanne wa kike. Hivi itakuwa:
(((3 x 2) +3) x 5) + 4 - 15
"Uchawi" uko kwenye zile digits ambazo nimeziweka kwa rangi nyekundu.
Kazi ya "2" ni moja. Unapofungua hizo brackets, 2 itazidishwa na 5 na hii itakupa 10. Hii ten itaazidisha idadi ya ndugu zako mara kumi. Kwa hivyo, kama ndugu wako ni watatu, Idadi hii itakuja 30. Tayari, unaona hapo "3" ndio idadi ya ndungu wa kiume ambayo itajitokeza mwisho wa hesabu.
place value ya ones/units itakuwa free na kuchukuliwa na idadi ya ndugu wa kike. Next ni "3." Kazi ya hii three ni kusafisha "0" yoyote inayoweza kuharibu hesabu. Kwa mfano, je, kama huna Ndugu wa kiume kutakuwaje? Hii ndio kazi ya hii "3".
Kama tulivyosema tayari, Kazi ya five ni fanya "2" iwe "10" na kusongesha idadi ya ndugu wa kiume kuelekea upande wa kushoto na kuacha place value ya wadada iwe "ones." Lakini hii five, ikizidisha "2", pia inazidisha "3" na basi ni lazima itolewe kwani inaongeza hesabu kwa "15". Hii kumi na tano tunaitoa na huu kwa kuondoa 15. kwenye hesabu.
Tatizo na hii hesabu ni kuwa haiwezi kufanya kazi ikiwa una idadi ya ndugu wa kike wanaozidi tisa, kwani place value ya kina dada ipo tu kwenye "ones" na inapozidi 9, basi itakuwa imeingi "tens" na ujanja wake utakuwa umeishi hapo.