Ulishawahi kukutana na hizi mambo?

Ulishawahi kukutana na hizi mambo?

Author

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2014
Posts
1,715
Reaction score
8,058
1. Uko unatembea zako au unafanya jogging ukapishana na mtu anafanya mazoezi ila hiyo harufu ya jasho inayotoka unayokutana nayo wakati mnapishana!...sijui kuna ambao hawafui nguo baada ya mazoezi au ni harufu jasho tu!

2. Kuna mtu hamjawasiliana naye kwa miaka mingi.Mara unaona anakupigia video call!...tena anapiga mara nyingi kama vile ni lazima upokee!

3. Mtu mmesoma naye shule ya msingi na mmepotezana kwa kipindi kirefuuuu...mara unaona ujumbe wake anajitambulisha, mnasalimiana na kujuliana hali. Hata siku haijaisha unaona ujumbe "naomba hata ya vocha"!.

4. Mtu kakupigia simu alafu anauliza "Nani mwenzangu?"

Yaaani, embu mdau weka mambo ambayo umekutana nayo yakakukeraaaaaa
 
Wale kila ukipita TU ukimsalimia akishaitika.....atakuuliza unaendeleaje????...vipi kazini bado upo pale pale????...... Hawa wanakera Sana maana mwingine anaulizwa na kazi Hana.......

Wale ukiingia baa TU akikuona Ni kosa.... Utafikiri nzi ameona mzoga kwa jinsi atakavyokuganda na kuja mezani kwako as if mlikuwa na miadi ya kumnunulia pombe....

Wale ambao kutwa kucha kujua ratiba za nyumba za watu.... Wako wangapi...wanakula Nini???? Nani anasoma wapi??? Nani hajitumi??

Wale ambao unapanda daladala anakaa mbele unakaa siti za nyuma ila saa ya nauli anamwagiza konda kwako.

Wale wa kukopa kila time anakupiga mizinga ilihali vipato vinalingana..

Yaani inshort sisi waafrica bado Sana mno.......
 
Yaaani wanakeraaaaa.....mnapokea salary pamoja kiwango sawa.Mnapokea leo kesho anakukopa....Daaaaaah;!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wanawake kwenye dala dala wanakera sana.
inshort huwa wanaamini ni HAKI yao kupata siti na wanaume wasimame
 
Back
Top Bottom