INAENDELEA...
Aling'ang'ana mno kunipigania kwa sababu alijua sikua na hatia, na alificha kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine, japo nilim-comfront mapema kabla ya chochote. Alijitetea kwamba walikua wamezinguana, hivyo alikua free kuwa na yeyote. Ilibidi niamini kwa sababu hata mimi nisingependa kukosa ule utamu. [emoji28]
Swali lilibaki kichwani ni Je, huyu mwamba alijuaje nakula pisi yake na tulikua very private? Mara zote alipokuja nafunga mlango, tunakaa ndani siku nzima, maana nilikua naandaa kila kitu mapema ili tusiwe na bughudha tukiwa kwenye tukio.
Nikamuuliza tena, hivi mwana alijuaje hadi nyumba nayoishi? At least ningeelewa kama tungekutana barabarani akaanza vita, ila lile jambo la kuibuka hadi geto lilinitatiza sana.
Muda ukaenda, mchana nikapigiwa simu na number ngeni ikinisihi nifike kituo cha polisi maeneo ya karibu na chuo. Kulikua na kituo kidogo cha polisi nje kidogo ya premises za chuo.
Ikabidi nimpigie Jessy haraka na kumuuliza kama ni yeye amepeleka taarifa zile polisi kwani nimeitwa muda si mrefu. Akaniambia we nenda, usiogope utakuta ujumbe wako. Nikajiuliza mengi mno, la kwanza kwanini Jessy kaamua kulikuza hili jambo na wakati nimemwambia fika kwamba sihitaji tafrani na mtu haswa kuanza kufikishana kwenye vyombo vya dola? Mimi ni mgeni nchi ya watu, sina hata wa kuniwekea dhamana in case of anything, kwanini hivi?
Basi bila hiyana nikatoka maktaba nikapitia geto kuchukua passport yangu na student ID nikaenda kituoni. Kufika tu wa kwanza kumuona ni Jessy!!!... Nikakosa amani kwa sababu ni mtu wa mwisho nilikua nategemea kumuona pale. Sikuwa namchukia kwa namna yoyote, kwa sababu nilijua jamaa kufanya vile ni ego ya kuwa mwananchi na ubabe tu wa kiume. Nilielewa sababu baadae.
Nikaingia tukasalimiana na officers na kuanza mahojiano. Nikaandika maelezo yangu japo niliomba haya mambo yasiende mbele kwenye uongozi wa chuo kwa sababu huwa yana adhabu zake zenye athari hasi kwenye maendeleo ya taaluma na nidhamu. Wakaniambia huyu bwana akikamatwa afanywe nini? Ukweli sikua na cha kusema, ukizingatia bado pia nilikua mdogo na uoga wa nchi mpya, nikawaambia mi nimemsamehe.
Wakaniambia watampa onyo kali na akirudia watamtia rumande. Tukamaliza pale tukaacha "kitu kidogo" (kama kawaida haya mambo nchi zetu yapo sana), tukaaga na kuondoka na Jessy. Tukawa tunaongozana huku sina kabisa story naye. Sikutaka mambo mengi, nikamwambia mi narudi zangu maktaba kumalizia assignment yangu. Kabla ya kuondoka akaniomba sana tuongee hata kwa dakika tano tu. Nikamwambia tutaongea jioni nikitoka maktaba.
Jioni kweli akanipigia, nikajaribu namna zote kumkwepa lakini alinisisitiza mno nikaona bora nimsikilize tu nijue anachotaka. Nikamuita maeneo ya karibu na maktaba akaja tukaanza kuzungumza. Swali langu la kwanza lilikua kwanini hukuniambia una mtu? Tena "violent boyfriend" namna ile? Kwanini unidanganye na kuhatarisha maisha yangu namna ile?
"Ni venye hujui tu Jimmy, I wish you knew how much detest that guy. Unajua mara ngapi ameniweka kwa ngori ka izi? Hii si mara ya kwanza ana-claim ati mi ni manzi yake". Akaendelea "Jimmy we mwanaume fiti sana, sikua tayari nikae nione mtu anakuchapa juu yangu na nikae tu ivo, no way. I've known you for few days but I feel I belong with you more than with him."
Nikamuuliza lakini si mtu wako? Akajibu "Ndio 'alikua' chali yangu sema sai ni kama tuko break kiasi ili ajisort juu ni mlevi na hakai anaeza change anytime soon." Sasa una mpango gani? Nikamuuliza. Akajibu "Kwanza huyu ni mtu nimejua for like 3 years now, tunatoka side moja huko Nax (Nakuru) na tumekuja chuo tukapatana hapa last semester, but honestly sina kitu ingine nataka na huyo mtu tena. Story yetu ni ka imeisha."
Tukaongea mambo mengi mno, na la mwisho nikamuuliza nani kampa taarifa za nnapoishi? Na alijuaje kwamba we're having 'a thing'?
"Huyo mtu kwao wako na doh, unajua ile doh fiti kiasi kwamba hapa chuo ako na mbogi (marafiki/washkaji) ye huwanunulia tei (pombe). Hata beshte yake moja anakaa kwa hio hostel yenye unaishi, namjua anaitwa Kevo. Huyo ndo alichoma, juu kuna siku nilipatana naye kwa gate nikitoka kwako."
Ohoo hapo sasa ndio nikaelewa kumbe snitch wangu aliyepeleka haya maneno ni jirani kabisa yuko upande wa pili wa korido ya hostel nayoishi. Nikakumbuka kuna siku nimekutana na mtu nje ananiangalia sana, mi sikutilia maanani kwa sababu sikuwa na kasoro yoyote, nikajua ni kawaida tu mtu kushangaa.
Wadau yule binti alifungua moyo wote siku ile, kwa mara ya pili kwenye maisha yangu "nikatongozwa na demu" [emoji23]. Najua sio kawaida ila ilishanitokea tena kabla ya kuanza chuo. Kwa namna nilivyomjua kwa kipindi kifupi tulichokaa pamoja, ukweli yule binti alinielewa na mimi hivyo hivyo. So the feelings were "mutual". Tukakubaliana sasa amchane jamaa live bila chenga, tena mbele yangu ili tujue kweli ile "situationship" yao imeishaaa.
Kabla ya kumaliza, akapigiwa simu na jamaa tukiwa pale pale, nikamwambia pokea tusikie anasemaje. Akapokea wakaanza kuongea:
Jessy: Sasa?
Jamaa: Fiti sana, uko?
Jessy: We sema chenye unataka.
Jamaa: Ni kama ulireport stenje (polisi) juu ya story ya Mtz? Ama si wewe?
Jessy: Si ndio, ama ulijua utachapa msee na you get away with it?
Jamaa: As in ni nini hu-get? Si nilikushow u-come kwa hao we sort this?
Jessy: Mi na wewe story yetu iliisha, na sina kitu nadai na wewe. I told you several times na kuonesha I moved on, lakini sijui nini mbaya na wewe hutaka kushikanisha.
Jamaa: We unajua unapenda kuongea mbaya but nikiambia matha ako anaweza kasirika mbaya?
Jessy: Hahahaha daamn kwani hajui?
Jamaa: Nakusubiri kwa nyumba.
Jessy: Utoke kwa nyumba yangu na kifunguo uachie caretaker ama nichange locks.
Jamaa: Fiti.
Conversation ikawa imeisha hivyo, mbele yangu. Short and sweet. Kwa akili ya kawaida tu, kama we ni mwanaume unajua kabisaaa hapa sina changu [emoji23].
Kweli nikaamini hapo mambo yalikua yameiva. Nilijisikia faraja kwa sababu alimkana jamaa mbele yangu nikiwa nasikia, na hata kwenye simu alikua amesave jina tu kuonesha kama ni mtu wa kawaida tu kama wengine. Nikamuuliza kumbe mlikua mnajulikana hadi nyumbani? Akasema ndio, aliwahi kumtambulisha kwa mama yake, walipokutana kwenye hafla moja huko kwao.
Na kuhusu funguo? Akasema alimpa spare in case amepoteza, au amesahau kitu, actually hata yeye alikua na spare key ya nyumba ya jamaa, ila alikua ameshakabidhi kwa caretaker wa nyumba.
Wadau hapo nikadhani kwamba mambo yameisha sasa, kumbeee ndio kwanza yanaanza. That guy was a psychopath, yaani alikuwa mwendawazimu kabisa tena akilewa.
Ngoja nivute pumzi tena, badae naendelea.