Ulishawahi kumuota nani humu JF?

Ulishawahi kumuota nani humu JF?

Martin Kemosabe

Senior Member
Joined
Jan 28, 2020
Posts
168
Reaction score
78
Hi guys

JamiiForums tunatumia ID ambazo si za kweli lakini pamoja na hayo kuna vitu maishani hauwezi vibadilisha wala kuviigiza na mfano wa kitu kimoja wapo ni ndoto huwezi igiza umemuota flani,huwezi igiza hili jambo hutokea automatical bila ya wewe kujua.

najua humu kila mtu anaota na ameshawahi kumuota member mmoja humu japokua hajawahi onana nae,kwa upande wangu nimeshawahi waota baaddhi ya memba humu sijawahi waona kwa sura wala live ila nimeshaonana nao ndotoni.

Maxence melo huyu nilimuotaga alikua headmaster wa shule ambayo mdogo angu anasoma,nilikua sifahamu kama max n head master siku 1 mdogo angu akwa anamuongelea head master wao alivyo mkali ktk kuongea akamtaja jina maxence melo,nikashtuka nikamuuliza tena head master wenu anaitwa nani? kanijibu Maxence Melo pale pale nikaingia google nikasearch pcha kisha nikamuonyesha kumuuliza ndio Huyu? akashangaa sana kisha akaniambia ndie basi kesho yake nikamwambia twende huko shuleni kwenu nikaongee na mkuu wako wa shule (lengo langu nimuone tu max maana simjui) nilifanikisha ikapita hiyo.

Numbisa kulikua na sherehe nyumbani na yeye ndio alikua mpambaji akaja na wafanyakazi wake basi nilitambulishwa kwake nilimshangaa sana maana si unajua tena mtu unamuona tu kwenye maaandishi kila siku,sema alikua bonge la dada duuu.

Gentamycine
alikua mpangaji mwenzangu siku 1 tukagombana kisa tu swala la kuchangia umeme,yani umeme umeisha yeye htaki kutoa wakati wengine wote tumetoa na sababu yake ya mgomo kisa tu eti hana Friji kwahyo hawezi toa hela ya umeme anadai TAA zake hazili umeme.

Fasi dwasi huyu nilimuota baada ya kututoka,kifo chake kilinihudhunisha sana,nilienda msibani na msibani niliumia sana hadi watu wakawa wanauliza marehemu na mimi tuna undugu wowote,basi ile siku ikapita

Baba swalehe nilikutana nae mwezi wa 12 ubungo stendi sikuwa namfahamu alinifata tu yeye mwenyewe na kujitambulisha kwangu kuwa anaitwa baba swalehe sema alikua anaongea kingeli hatari sana nilifurahi sana kuonana nae.

Shunie/heaven on earth/Ram/depal/khatwe/atoto/manengelo ni memba niliowahi waota kwa nyakati tofauti siku tofauti ni wapenzi zangu hizi ID nilizotaja kuna ambao wameshazibadili nawajua wote ila ndoto zangu juu yao nilizipata wakiwa na id hizo nilizotaja hapo juu.

Faizafoxy alikua shangazi angu walishagombana zaidi ya mara 1 na baba angu kwa sababu zao wenyewe

Pascal mayala
jirani yetu home

Hao ni wachache sijui wewe ulishawahi kumuota nani,ktk wote hao hamna niliyemsingizia ila narudia kusema kuwa hii ilikua ni ndoto tu na si kweli.
 
Akili yako yote imefunga ndoa na huu mtandao.
Sijawahi kumuota yeyote humu wala kumfikiria nje ya hapa....yote huishia hapa hapa kwenye uwanja Wa udanganyifu....unamuotaje feki pipo mkuu?
 
Back
Top Bottom