Chambichambi
Senior Member
- May 23, 2022
- 139
- 229
Habari Watanzania!
Leo nina stori ya kweli ambayo imetokea katika maisha nikiwa mkubwa hivi. Basi bwaana baada ya kumaliza masomo nilianza vijikazi vya hapa na pale kuendesha maisha yangu. Nilipigana kama miezi 5 bila mafanikio.
Niliamua kwenda mwambao wa ziwa Victoria kuangalia fursa zingine za kufanya ili kutimiza ndoto yangu ya kumiliki mihela. Nikafikia kambi moja ya uvuvi wa dagaa nikajieleza kwa wavuvi kuhusu kutaka kujifunza uvuvi.
Nilifanikiwa kupata mtu ambaye alikubali kunifundisha japo nilikuwa sifahamiani na yeye. Basi jamaa alinitambulisha kwa wenzake wanaotega nao mtumbwi mmoja. Baada kula saga nilienda nikakaa sehemu nikalia sana lakini nikasema yote maisha.
Basi baada ya siku mbili ilifika mbala mwezi ya saa 5. Tukaenda ziwani sasa siku ya kwanza. Nakumbuka siku hiyo tulienda maji ya meli, ziwa lilikuwa limetulia kama mkeka. Tukatega kesho yake mimi mwanafunzi nilipewa Tsh 27,000 na mboga kama sado ya dagaa mbichi. Badae nikawa mzoefu nakaanza kwenda visiwani.
Nakumbuka ilikuwa mwaka jana nikiwa kisiwa fulani niliugua miguu mpaka hata kutembea nikawa siwezi. Nilijikaza kisabuni lakini wapi. Nikatumia kila kitu miguu bado. Nikaomba msaada nyumbani nikapewa nauli nikaenda home.
Aiseee nilivyofika kila mtu alikuwa anashangaa na kuniuliza kuwa nimefanya nini? Dah! Kwakweli sitosahau kipindi hicho nilikuwa sipati usingizi usiku miguu ilikuwa inauma kinoma.
Baada ya hiyo hall kuna ndugu baadhi walianza kunichukulia kama mtu ambaye sijiwezi kwani nilidhihirisha kuwa kazi za uvuvi ni kazi za watu duni. Sasa kila siku ikawa ni mabango na kauli za kejeli kama, "elimu yako haikusaidii kitu". Sema niliumia sana mpaka nikaamua kujaribu kujua. Niliamua kula vidonge 26 na konyagi kubwa ili nife.
Asikwambie mtu nilikaa ndani siku 5 nikisubili kufa bila mafanikio. Badaye nilijikuta nimetundikiwa drip za maji huku nikiuliza huku nimefikaje?