Wala simalumu jamaa, wewe move on wacha kulia lia mtoto wa kiume.
Ni kawaida watu akipata nafasi mahala atakutana na watu wanao speak the same language, watu wa haiba yake. Hata sehemu za kuonana hazitakua sawa na huko awali. Kiufupi mtu akipata (hata wewe) utabadili mfumo mzima wa maisha.
Kipindi yuko maskini story zilikua za level yako na jokes za level ya kimaskini, now story zitakua tofauti tu, akija hapo aanze kuongelea story za magari, ujenzi wa nyumba na biashara zake utakuja kufungua uzi hapa kuwa jamaa anajidai (kumbe mwenzio ndio maisha yake saa hizi)
Hapo option na wewe pambana utusue, hapo mkionana mtaongea lugha moja
Sikubaliani na hili ni aina ya mtu tu alivyo, wengine ni ulimbukeni wa mafanikio na wengine wana roho mbaya za chini kwa chini zilizojificha chini ya kivuli cha umasikini.
Ndio maana werevu husema "pata tuijue tabia yako".
Labda nilete mkasa wangu ambao unafanana na mleta mada kwa ufupi, kipindi nipo chuo nlikuwa na washkaji kama wanne hivi ambao tulikuwa tunaishi ghetto moja, tulikuwa kama ndugu wa kuzaliwa, utani kama wote kama vijana, kula pamoja, kwenda sokoni pamoja, kuburudika pamoja, kusoma pamoja. Tulifanikiwa kumaliza chuo tukarudi mtaani , kwa mda ambao wote tulikuwa ma jobless tuliendelea kuwasiliana hapa na pale , mara kwa mara kuendeleza urafiki wetu.
Kipindi kikapita miongoni mwetu baadhi wakaaza kupata michongo(kazi) japo kazi hazikuwa permanent ila wakaanza mabadiliko ya hapa hapa na pale.
Bahati mbaya au nzuri mimi ndie niliyepata kazi wa mwisho kati ya hao washkaji.
Sasa kuna mshkaji ambae aliepata kazi kabla yangu mimi alikuwa nae akinilalamikia kuhusu washkaji ambao alikuwa nao katika mihangaiko wanampotezea kwa kuwa wao walifanikiwa kabla yake.
Alivyokuja kupata yeye nae akaanza kunibadilikia mie ambaye nilikuwa mshkaji wake ambaye alikuwa akinilalamikia juu ya washkaji zake waliompotezea katika mihangaiko yake.
Alivopata kazi alinipigia simu kuwa ile ishu imetiki mzee. ""Nikampa hongera mzee umepambana "Mungu akutangulie.
Kipindi cha mwanzo alivyopata kazi , tukawa tunawasiliana kama kawaida, kumbuka mimi hapo bado najitafuta sina hili wala lile"
Kadri siku zinavyozidi kwenda akaanza kuonesha mabadiliko, kiasi ya kwamba nikimpigia simu akipokea dakika mbili anakukatisha na kukwambia nitakurudia, hakuna cha kukurudia wala nini, anapiga kimya tu.
Na wala sikuwahi kumuomba chochote kinachohusiana na hela wala nini, au kumdadisi kuhusiana na ujira aupatao kazini kwake.
Maana naelewa hata iweje kuna maswali ukimuuliza mtu automatically yatamkwaza, sikuwa mtu wa aina hiyo.
Mwanzo nlikuwa nachukulia kawaida labda pengine mwanangu kazi nyingi, nikapunguza kumpigia simu, nikawa namtafuta siku za weekend nako pia akawa ananipotezea ukiongea nae dakika mbili anatafuta sababu hapo hapo za kukukacha, nikasema kimoyomoyo , kumbe anajiona keki sasa😄nikapiga zangu kimya, na kuendelea na mihangaiko yangu ya kupambana kwa mda mrefu approx. miaka miwili.
Nikaja kupata mchongo flani wa mda, baada ya kusikia kwa watu kuwa jamaa flani amepata kazi, akaanza kunitafuta, namie nikaanza kujifanya nna bize nyingiiiiiiii😂😂
Naongea nae dakika mbili na kumwambia subiri kdogo nitakupigia😂😂 alaf nakacha kimyaa.
Mungu sio Athumani, kukaa kdogo nikaja kupata kazi ya kudumu serikalini tena taasisi nono, kuja kusikia zikawa simu zinafululiza kana kwamba vile anataka kuyajua mambo yangu, ila anakutana na malalamiko tu nikumuaminisha kuwa bado nipo kwenye mchongo ule ule wa awali nalia njaa tu, ila nafsi yake haiamini bado maana alishasikia kuwa fulani sasa hivi ni mtu mwengine.
Ikiwa yeye bado yuko katika kazi ile ile ya mkataba anaisongesha(Namuombea kheri).
Kati ya wale washkaji wanne mmoja tu ndio nawasiliana nae mara kwa mara licha ya kuwa nae alitangulia kupata kabla yangu.
Nachotaka kusema asilimia kubwa ya washkaji tuwe nao tu ila wengi wao sio, hata awe analia lia vp akipata nae anaendeleza vile vile.
Mpaka sasa sio mtu wa marafiki, mda mwingi nafocus mambo yangu yanayonihusu mimi na familia yangu.