Ulishawahi kuwa addicted?

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Facebook kuna mchezo unaitwa Farmville, kuna wakati nilikuwa addicted kabisa, nilikuwa ninapanda mazao kuhakikisha baada ya masaa matatu yatakuwa ni ya kuvuna, nitaharakisha kila ninachofanya ili niwe free baada ya masaa matatu. Kuna wakati nilikuwa ninaamka katikati ya usingizi ili nivune mazao yasioze. Hapo ndipo nilipogundua nina tatizo, nilijitoa. Siku hizi FB ninakwenda kuchungulia tu.

Uliwezaje kuacha addiction yako?
 
Mimi mpaka sahivi nipo addicted na video games nikijifungia kucheza Ps3 huwa nasahau kula na ninaweza nikakesha nacheza tu nashindwa kuacha sababu nayapenda mno
Nephew wangu alipata constipation kwasababu ya kudharau haja kubwa akiwa kwenye video games. Siku alipata choo kiliblock si kwa jiwe lile, ilikuwa shughuli😛
 
Addiction yangu mpira wa miguu tuu, achilia mbali Manchester united timu ninayoishabikia ila imefika mahala naangalia ligi yoyote inshort nikigundua Kuna mechi yoyote inachezwa iwe ligi ya Italy, uholanzi, ufaransa au Spain nimo.

Hapa Kama leo imefika ijumaa nikiingia ndani ni mpira tuu mpaka j3 kazi yangu kubadili tu stations za mipira, hii addiction Wala sijutii inanisave na mengi ya walimwengu ingawa mahusiano yangu ya mwisho yalikufa kutokana na mwenzangu kushindwa kutokana na mpenzi yangu mpira yaliyopitiliza mipaka.

Napoongelea mpira wa miguu namaanisha kuangalia mpira, kubishana kuhusu mpira nipo kwenye groups kama 4 hivi za soccer, mavazi yangu ya kushindia nyumbani na mishemishe za hapa na pale kwa kiasi kikubwa ni jezi za mpira, marafiki wangu wengi wamebase kwenye mpira, Mimi sio muongeaji asili yangu Kama sio kubishana mpira basi tunaeza kukaa kimya hata masaa mawili usiponiongelesha, kwa vijana wa Sasa wapenda mpira Kuna kitu kinaitwa FPL ( Fantasy premeir league) humo namo nimo hii ndio imenishika kabisa.

Hiii addiction inaenda sambamba na muziki simu yangu ina application ya Spotify nikiweka earphones masikioni nisahau kabisa ukipiga simu sipokei hata awe ya boss.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…