Ulishawahi kuwa na rafiki wa jinsia tofauti mliyeshibana sana?

Ulishawahi kuwa na rafiki wa jinsia tofauti mliyeshibana sana?

Umemkuta mumeo na rafiki wa kike au unaongea nadharia tu? Let's be realistic jamani, hii kitu ni ngumu ku-maintain watu wakiingia kwenye ndoa. Kila mtu anatamani kuwa na mtu wake peke yako...
Ngumu kwako wewe. If you have open mindset with no insecurities mbona kawaida tu, Maisha yanaendelea bila worries.
 
Ngumu kwako wewe. If you have open mindset with no insecurities mbona kawaida tu, Maisha yanaendelea bila worries.
Sidhani kama ni sawa kuwalaumu wanaoshindwa, watu tupo tofauti ndio maana kwako ni sawa na kwangu sio sawa. Muhimu ni kuheshimu maamuzi ya huyo mwanamke, hata mimi kama wife ana rafiki wa kushibana nitamwambia waache mara moja, hakunaga urafiki wa me na ke just like that, end of it watamegana, na umeona hapa watu wametoa shuhuda zao.
 
Mimi nimewahi bro lakini ni kama kutembelea muwa kama fimbo lazima utaula tu ndio kilichonitokea all in all bado ni washkaji kwa sasa ila sio kiviile [emoji28]
 
Sikuwahi mtamani, sababu ule ushkaji na ukaribu tuliokuwa nayo nlikuwa namwona Kama Mwanamke mwenzangu sometimes. Nikiskia mrejesho wa mdinyo ilikuwa Ni siku ya kicheko.
Kumbe huwa mna wachukulia kama mashoga zenu...asee!!
 
Umenikumbusha msh'kaji wangu G,daah!!! Tulikuwa zaidi ya marafiki buanaa pale SJUT Dodoma,.yaani ni yule msh'kaji ambaye akisafiri akachelewa kurudi chuo na assignments zinatakiwa basi nakesha Google namfanyia na namkusanyia kabisaa and likewise,.mmoja kati yetu akiwa na changamoto yoyote ile hata ya mahusiano basi tutaumia wote,hadi kupiga [emoji482][emoji482] tupo wote in short tulikuwa karibu kuliko tulivyokuwa na wapenzi wetu,.

Sijui kwann urafiki wetu ulikuja kuisha namna ile [emoji17]ila najua ulikuwa damu yangu kinyama,.popote ulipo nakutakia tuu yenye kheir,tulibebana sanaa G,. anyway one love [emoji177]
Pindi la DS mule MH mnakaa wote mnatosha daaah shule hizi...!
 
Alikuwepo mmoja tangu kakiwa kabinti ka miaka 14 anaanza form 1, alinizoea mnoo akizinguana na boy ake lawama ananiletea Mimi, akiwa hampati hewani mi nakua m'badala, wakaachana nilipata kazi sana kwa kweli kumuweka sawa adi leo ananishukuru maana alikaribia kujiua.
Tuliendelea ivo adi kamaliza chuo kapata kazi, nilivyooa alibadilika sana hakua tena na furaha na mimi, anadai mbona yeye ananishirikisha habari za mahusiano yake mi nilikua simshirikishi nkamwambia alipata mimba ikabidi nimsogeze tuishi wote lkn bado kawa na hasira.

Nae akaja akaolewa anaishi na mmewe siku ilitokea tukakutana kwenye sherehe akaniomba nimrudishe home maana gari yao ilikua mbovu na mmewe yupo shifti ya usiku, kufika getini kwao kimasihara tukaharibu urafiki wa kaka na dada, kesho yake ndio anafunguka alikua anatamani sana nimuoe lkn alihofia nilimzidi sana umri na alikua akiniheshimu sana.

Kuna watu mtaani ukiwaambiwa hatukua na uhusiano hawaamini kabisa lkn ukweli ndani ya miaka 12 hatujawahi hata kutongozana.
 
Hata mm nilikuwa nae best yangu mzuri kinyama. Tulielewana mno tunaelezana kila kitu mpaka usiku wa manane ikitokea nimeota ndoto iwe mbaya au nzuri nampigia tunaongea.

Ukweli alikuwa rafiki yangu sana. Akapata mchumba nikaonywesha na akamtambulisha kwangu kwamba mm ni best yake, mipango ya harusi ikafanyika kiasi cha kumsaidia mchumba wake kutafuta gauni la Harusi sambamba na kulipeleka kwao bibui harusi siku mbili kabla ya tukio.

Yaani nilijitoa kwa hali na mali kwa jairi ya best yangu tena nikiwa na furaha.

Lakini baada tu ya ndoa kupita mambo yalibadilika. Mke akaona tunadanganya ikawa zogo mume ananyimwa huko. Ndani patashika vurugu mtindo mmoja.

Nikaona isiwe shida nikakata mawasiliano na best yng kipenzi ili tu kunusuru ndoa yake.

Ila na mm namkumbuka sana kwake nilikuwa na amani sana na furaha.
 
I had a friend, wa kike pale chuoni cbe. Alinifaa sana. Alinishauri mambo mengi sana na nilimwamini kiasi cha kumwambia kila kitu changu. Chochote alichonishauri niache, nilifanya mala moja. Alilazwa REGENCE kwa ajili ya kujifungua, nilimtembelea mala nyingi kumjulia hali just for love, mpaka kuna mda nikifika ndugu wanashangaa. Nilimpenda sana yule dada as a friend. Alinifaa sana. Urafiki ulikatika alipoenda [emoji631] us. Mawasiliano yalikuwa finyu. Its almost 11 years now but bado nakukumbuka. Popote ulipo B, jua nakukumbuka sana na nathamini mchango wako kwangu.
 
Habari zenu wakuu,

Nimemkumbuka kaka fulani tulikuwa marafiki sana tangu nikiwa secondary. Kwa miaka 10 alikuwa mtu wangu wa karibu sana, mshauri wangu kwenye kila Jambo.

Kiasili Mimi ni introvert, sipendi mashost, mashoga wale wakunijua kiundani. So kuwa na this guy ambae nlikuwa namwambia issue zangu ilinifanya
Siku hizi urafiki wa hivyo wa kweli ni nadra sana, wengi sasa hivi wapo kimaslahi, bahati ukutabe na mtu mnaeendana hivyo.
Jamaa hakuwahi kujaribu kuonja tunda?
Maana wanasema mua ukiutumia kama fimbo siku ukizidiwa njaa utaula tu....
Hongereni kwa urafiki mzuri.
 
Ninao marafiki wa kiume wa karibu katika nyakati zote za maisha tangu shule ya msingi.
Wako ambao tumekuwa familia marafiki.
Heshima kwao wote. Aliyekuwa mpenzi kisha mume nilimtaarifu mapema kuwa wapo na nashukuru ananielewa.
Na wao walijua mahusiano yangu na wengine tumeextend urafiki umekuwa wa familia. Nguo na viatu vya kitchen party na send off niliwaambia wanichangie na wakanipa.

Mmoja wa karibu sana mchumba wake alijitahidi sana kuachanisha ukaribu na bahati mbaya huyu rafiki alifariki soon baada ya ndoa yake. Mpaka leo mimi ni sehemu ya familia yake, kidogo nikipata nawatumia. Wadogo zake wakiwa na shida wananipigia. I miss him so much.

Marafiki waliopo tunaendelea sema kwa sasa tuko mbalimbali.

Sikuwahi kuwafikiria kama wapenzi kwa sababu wana heri nyingi lakini wana kasoro za msingi kwangu kuwa wenza na bahati wako wanawake wanamudu vizuri hivyo ambavyo mie siwezi.
 
Back
Top Bottom