Ulitumia jitihada, njia au mbinu zipi kupata ajira au kujiajiri?

Ulitumia jitihada, njia au mbinu zipi kupata ajira au kujiajiri?

bay_zooh

Member
Joined
Jan 27, 2025
Posts
43
Reaction score
65
Habari za wakati huu wanaJF,

Naombeni mnisaidie wenye uzoefu na hili.

Pengine kwenu wanaJF mlitumia njia zipi kuweza kupata ajira au kujiajiri, nimeuliza hili kwa sababu naona maisha yanazidi kunipalia, binafsi nimehitimu shahada ya mambo ya uchumi na takwimu nimejitahidi kutafuta ajira kwa kila namna lakini bado mambo si rahisi, yaani hata ya kujitolea sjafanikiwa na kujiajiri ni vivyo hivyo mambo ni vice versa.

Mpaka nahisi labda kuna mahali nakosea.

Majukumu yamenijaa, masimango ya wanajamii hahhah dah mpaka nahisi kukata tamaa lakini ndo hivyo mtafutaji hachoki.

Naombeni ushauri wenu pengine naweza kuinuka na ari mpya.
Natanguliza shukran.
 
Nilipewa laki moja nikaanza na mtaji wa laki baadae nikapata tena laki nikapata akili nikaenda kulipia kama ada ya kuchukua bajaji ya mkataba 🤔🤣japo sahivi nipo tu mkata majani na ni degree holder

Ila usichoke
Nashkuru.
 
Ajira yangu ya kwanza nilipata Connection nilipata ya kazi ya kujitolea mahali Fulani.

Nlijitolea miaka mitatu nalipwa 80,000/= kwa mwezi.

Baadae wakati nafikiria kuacha nkapewa mkataba wa ajira Miaka mitano mshahara ukawa 980,000/=

Sikujui nifurahi au nfanyeje nkaendelea na kazi pale.
Ikawa hivyo
 
Hongera sana.
 
Watanionaje itakulaza njaa ! Achana na hayo makaratasi,,,, nenda site komaa, endesha hata mkokoten, choma mahind Road, tengeneza mihogo, mishkak vitafunwa uza,,, inategemea na eneo ulilopo ,,, point yangu ni kwamba usichague kazi kama unajijua ni mtoto wa mkulima
 
Back
Top Bottom