Ulitumia jitihada, njia au mbinu zipi kupata ajira au kujiajiri?

Ulitumia jitihada, njia au mbinu zipi kupata ajira au kujiajiri?

Watanionaje itakulaza njaa ! Achana na hayo makaratasi,,,, nenda site komaa, endesha hata mkokoten, choma mahind Road, tengeneza mihogo, mishkak vitafunwa uza,,, inategemea na eneo ulilopo ,,, point yangu ni kwamba usichague kazi kama unajijua ni mtoto wa mkulima
Nashkuru sana.
 
Kila la kheri katika mapambano yako mkuu..

Usijaliii watu wanaongea nini kuhusu wewe.

Wewe pambana tu.
 
Fuatilia hizi nafasi,,Chagua Ufundi wa magari na umeme wa magariView attachment 3225934
Screenshot_20250202-143025.jpg
 
Tafuta passport, Andaa documents zako vizuri, Fanya research ya kutosha.

Kasake maisha ughaibuni.

Maisha si Tanzania tu.
Kwakweli angekuepo au ingekuepo njia mahususi ya kufanikisha hili ingekua nzur sana ...kukaa hapa nchini naona Haina mana Wala faida kwa Sasa kama vijana wanajipaka matope wanapita mbele ya rais
 
Weka vyeti kabatini, pambana na maisha sasa,
1. cha kwanza zingatia upate uhakika wa kula milo mitatu, uhakika wa kulipa kodi ya pango umeme na maji, ukiweza hiyo hatua ndio unaenda na hatua nyingine.

2. Usisikilize maneno ya wana, wengine huwa wanavunja moyo sana, jipambanie kipekee yako

3. Usijifananishe wala kujilinganisha na wengine hiyo itakuvunja moyo, kumbuka kila mtu ana namna yake ya kuvuka kwenye jambo.

4. Tafuta mwanamke muelewa anayejua, hatua za maisha achana na wale wanajua mwanaume ni baba yake wake wa kufikia
 
Nilipewa laki moja nikaanza na mtaji wa laki baadae nikapata tena laki nikapata akili nikaenda kulipia kama ada ya kuchukua bajaji ya mkataba 🤔🤣japo sahivi nipo tu mkata majani na ni degree holder

Ila usichoke
Bajaj ulienda kuchukua wapi kwa mkopo?
 
Mimi baada ya kumaliza chuo 2019 kwa ngazi ya diploma

Nikawa Sina mishe yoyote mtaani ndipo jamaa akanambia twende tukauze mifuko sokoni temeke sterio

Nashukur Mungu nikawa napata pesa ya kula, kuvaa Na malazi na hata pesa ya kwenda kufanya usaili pia

Ila changamoto hazikosekani maana watu hasa majirani pale mtaani wakawa wananicheka eti kusoma kote kule naishia kuuza mifuko

Mungu ni mkubwa nikaja kuajiriwa serikalini Na diploma yangu

Washkaji wote waliokua wananibeza hawaamini kilichotokea wao Bado wapo tu mtaani hawana mbele Wala nyuma
 
Kazi yangu ya kwanza maana siit ajira niliipata hivi.

NNilikuwa na tabia ya kuzungukazunguka kuangalia Fursa nikaona Gym mpya imefunguliwa nikawaza nikaombe kazi au nikaulizie kama anataka matangazo ya picha Graphis kwenye gym.

Nikaenda nikakuta msimamizi nikamwambia ninashida na Boss mwisho akanipa namba yake nikamtumia sms nataka kazi ya kusomamia GYM sikai mbali na blaa blaaa akanijibu njoo jioni nikaenda anakiambia hapa kuna mtu ila kuna kazi ABC... unaweza ofisi ni City Center uje kesho mpogie ABC.. nikafika kesho yake nimepigilia kwa mara ya kwanza nikawa ofisini.

Kwa mwezi mshahara ulikuwa 200,000 ila hio ilkuwa kama milioni kwangu kwa Doso nililochezea mtaani aisee.....Nilifanya kazi kama miaka miwili kikaenda kikashuka sasahivi siamini kama kwenye akiba ya mwezi huu nimeweka 500,000 na kuingiza 50,000 kama kiposho cha kazi kwa siku kawaida.
 
Baada ya kumaliza chuo bhn nilitokwa na chozi 😂 nikifikria maisha nayoenda kuishi aseeh

Nilipata kuwa na wanafunz waliokuwa na sup kuanzia tatu, wengi wao nikiwa mwalimu wao nilivuna hela ya kula , vocha , na malipo nilitaka niyapate direct kwa wazazi wao.....

Nikatoka hapo nikafungua business, aseeh niliona moto, mtaji hautoshi Kodi ya nyumba ya biashara ukikaa hivi Kuna mambo kama mia mbili..... Hapa nilibugi step coz nilitaka kuwa na mamalishe standard tuu nikakimbilia kuuza nguo..... Biashara ikafa!

Nikapata kazi au internship sijui niweke vipi vyote sawa, nikapiga job nikapiga job, mshahara ulikuwa wa kawaida tuu Ila nilikuwa naipenda kazi so far nimefanya mpaka pale biashara/ kampuni ile ikastop!

Nikarudii kuwa assistant manager bar, nako nimeuza bia hizi nimehangaika hapo mpaka sasa nakaa tuu hapo still nakomaa kiaina

Kikubwa upate kuishinda kwanza njaa, Kodi maake njaa inauma, bado Kodi huna pa kukaa utadata, hivyo tuu mkuu
 
Kazi yangu ya kwanza maana siit ajira niliipata hivi.

NNilikuwa na tabia ya kuzungukazunguka kuangalia Fursa nikaona Gym mpya imefunguliwa nikawaza nikaombe kazi au nikaulizie kama anataka matangazo ya picha Graphis kwenye gym.

Nikaenda nikakuta msimamizi nikamwambia ninashida na Boss mwisho akanipa namba yake nikamtumia sms nataka kazi ya kusomamia GYM sikai mbali na blaa blaaa akanijibu njoo jioni nikaenda anakiambia hapa kuna mtu ila kuna kazi ABC... unaweza ofisi ni City Center uje kesho mpogie ABC.. nikafika kesho yake nimepigilia kwa mara ya kwanza nikawa ofisini.

Kwa mwezi mshahara ulikuwa 200,000 ila hio ilkuwa kama milioni kwangu kwa Doso nililochezea mtaani aisee.....Nilifanya kazi kama miaka miwili kikaenda kikashuka sasahivi siamini kama kwenye akiba ya mwezi huu nimeweka 500,000 na kuingiza 50,000 kama kiposho cha kazi kwa siku kawaida.
Wazo zuri
 
Back
Top Bottom