Dah,
Story yangu ndogo kutoka maisha ya ujanani.
Umenikumbusha wakati bado mdogo, teenage years, siku moja nilipiga kipensi cha jeans ya kuchanikachanika, nikawa nasindikiza mtoto mkaliii mtaani. Alikuwa anarudi kwao baada ya kunitembelea na kumaliza yetu.
Basi nilivyorudi kumsindikiza yule girlfriend wangu, mdada mmoja mkubwa wa mtaani, bonge la sister du, akawa kama haamini mambo yangu yale, alikuwa ananichukulia poa kaniona nakua tangu mdogo.
Yule sister du dada mkubwa wa mtaani akashindwa kujizuia, akaniita, akaniambia yule msichana wako nzuri sana, siku nyingine ukiwa unamsindikiza uvae vizuri zaidi na wewe usivae kama vile jeans la kuchanikachanika (siku hizo kuvaa jeans la kuchanikachanika ilikuwa inaonekana uhuni sana, haikuwa kawaida kama siku hizi).
Akasema haileti picha nzuri.
Halafu mimi nilimchukulia poa tu yule msichana wangu. Na yeye mwenyewe alikuwa poa tu na vile nilivyokuwa.
Nilimnasa vipi?
Alikuwa anapenda mambo yangu mengi tu, stories zangu, mambo ya muziki, mambo ya public speaking. Alikuwa anapenda sana king'eng'e changu na vitabu nilivyokuwa nasoma.
Alikuwa anasema nafanana na Denzel Washington katika "Mississippi Masala".
Kifupi alipenda akili zangu zaidi kuliko hela kwa sababu wote tulikuwa wadogo hata hela nilikuwa sina hivyo, hapo hata kazi sijaanza.
View attachment 3269498