Mteja aliyenipeleka kwa wakili kwa ajili ya Radio
Nilipomaliza chuo, nilikuwa natafuta mteja redio, nikapata mteja mmoja wa ajabu sana. Nilikuwa nauza redio kwa shilingi elfu 30 tu, lakini jamaa akaniambia, “Twende kwa wakili tusaini mkataba!”
Nilidhani anatania, kumbe yuko siriazi kweli ! Tukajikuta ofisini kwa wakili tukisaini mkataba kana kwamba namuuza gari au kiwanja! Wakili akatuandikia makubaliano rasmi kabisa, nami nikapewa nakala yangu. Nilibaki nashangaa.
Safari ya biashara Iliyoishia porini
Nilikutana na muuzaji mmoja kupitia Facebook, akanielekeza tukutane sehemu flani, Tulipokutana, akanambia tupande boda tukakague bidhaa. Safari yenyewe ilianza kwa matumaini, lakini kadri tulivyozidi kwenda, tulikuwa tunazama bush, watu wanahesabika njiani, Kwa hali ya usalama nchini, moyo wangu ukaanza kudunda nilidhani wanaenda kunipora hela niliyobeba au kuniteka.
Nikamdanganya kuwa nimebanwa na haja, akasimamisha boda. Niliposhuka, sikurudi tena. Nikaingia kichakani na kutafuta njia ya kutokomea. Simu ikaanza kuita, sikupokea, na hatimaye ikazima kabisa.
Usiku nikamwandikia ujumbe nikamweleza kwa uwazi kuwa sikuweza kuendelea na biashara kutokana na sababu za kiusalama. Jamaa akajibu kwa kicheko tu, lakini mimi nilikuwa makini, maisha kwanza!