Lovelovie
JF-Expert Member
- Oct 2, 2021
- 12,582
- 26,053
Mim napenda kuheshimu na kufuata masharti nikiwa kwa watu vivo hivo nikiwa kwangu nahitaji heshima na nyumba yangu.Oh my God, mbwa anaingia na kutoka nyumba tunayoishi, room mate kamleta mbwa mdogo wa kucheza nae, shughuli si ndogo hii!! kuna muda tulienda kikazi mkoa x kwa miezi mitatu, niliishi na jamaa anapenda sana mbwa, siku ya pili kaleta ki puppy kimbwa kidogo anakijali kama mtoto wake vile, kucheza nacho kama rafiki, n.k. ishu ilikuja hiki kimbwa kaanza kukiingiza ndani, ebwana ee hapa ndipo tuliposhindwana, nipo naangalia tv mara naona kuna ulimi unapenyezwa katikati ya vidole vya mguuni, nasisimka kwa hofu kucheki chini ni kimbwa, duh!
Room mate asie na mishe, nipo kitaa hapa nina geto langu baada ya kumaliza chuo, kuna jamaa aliomba aje mjini kupiga mishe nimsaidie ajishikize kwa siku 2 ama 3 atafte chumba, cha kushangaza jamaa kaja na redio kubwaaa na begi la kawaida, nikiondoka namwacha na wala hajishughulishi zaidi ya kusikiliza muziki, chakula juu yangu, umeme juu yangu, nikaona huu uduanzi sasa, nilimwambia atupishe kidogo nataka niishi na dem wangu.
Kabla ya yote ni bora nimwambie mtu masharti ya nyumba yangu, nilijifunza mwanzo.