Uliwahi kulilia mapenzi?

Uliwahi kulilia mapenzi?

🤣🤣🤣 unapenda nilizwe na mapenzi dogo?? Haya ngoja nikupe ushindi wa mezani.!
Jana nilikua napitapita mitaa ya jf nikakukuta mtaa mmoja unajimwambafai kua huwezi kulia kisa kuachwa sasa hapa nawaza kama uliacha na ukalia what if ukiachwa? Si tunajenga matent hapo kwako mapema tuu.
 
Jana tu nimelia. Nilikuwa nahisi kuanza kumchoka mwanamke wangu. Nilikuwa namtafutia visababu nimuache ila hakujaa. Akaja kujaa majuzi. Alifanya kosa la kupekua simu yangu kwa siri, akapiga picha vitu alivyokuwa na mashaka navyo akakaa kimya.

Zimepita siku kama tatu akaniita kwa unyenyekevu tu na kuanza kuniuliza,nilimtukana sana kwa kunipekua, na nilidhamiria itakuwa ndio sababu ya kumpiga chini kwakuwa nilihisi simpendi kama mwanzo. Aliniomba msamaha ila nilikaidi kabisa na kumpa maneno makali, ikumbukwe siishi nae.

Nimekuja kulia baada ya yeye kuniandikia sms ndefu sana akisema leo (ambayo ndio jana) kuwa ndio amepanda gari anaondoka kabisa kwakuwa nimegoma kumsamehe, ila akanikumbusha kuwa ananipenda sana. Kaamua kuondoka na kurudi kwao na kazi kaacha alipokuwa anafanyia. Nilihisi uongo japo roho ilianza kuniuma. Nikaenda kazini kwake kuhakikisha, sikumkuta na hakuna mwenye taarifa. Ikabd niende anapokaa, nikakuta kweli kaondoka na chumba kaachia.

Nililia sana, nikagundua nampenda ila kibri tu cha kumuona si chochote. Baada ya kumpoteza ndio naona thamani yake. Nilimpigia simu tukaongea, kasema ameamua kurudi kwao tu awe mbali na mm. Tumeshafanya mambo mengi na yeye, zawadi alizonipa, upole, ukarimu na utiifu wake kwangu ndio mambo yanayoniumiza. Rafiki zake walikuwa wakinieleza juu ya jinsi alivyokuwa ananipenda na kunielezea kwao.

Ikabidi nimuombe msamaha kwa kila kitu, nilimwaga machozi. Bahati nzuri amenisamehe na ameniahidi atarudi kwa ajili yangu.

Nimepanga kuishi nae, nimegundua ni mwanamke wa kipekee sana.
Hongera sana kwa kutambua madhaifu yako yafanyie kazi, ukweli ni kwamba mwanamke bora/mwanaume bora huwa haji maishani mwetu mara mbili… Utaupgrade uwezavyo, ila kamwe huwezi kuziba gape la mwenza bora.
 
Hongera sana kwa kutambua madhaifu yako yafanyie kazi, ukweli ni kwamba mwanamke bora/mwanaume bora huwa haji maishani mwetu mara mbili… Utaupgrade uwezavyo, ila kamwe huwezi kuziba gape la mwenza bora.
Hakika sijui kwa nini huwa hivi, mtu bora huja mara moja na ukishampoteza ndio basi imeisha.
 
Jana nilikua napitapita mitaa ya jf nikakukuta mtaa mmoja unajimwambafai kua huwezi kulia kisa kuachwa sasa hapa nawaza kama uliacha na ukalia what if ukiachwa? Si tunajenga matent hapo kwako mapema tuu.
Mi nachangamsha kijiwe hapa wala simaanishi, ila yule jamaa nilimkosea nafsi imenisuta sana ndiomana nilimuacha nikalia kwa huzuni..!! Ila namrudia nimegundua alikuja duniani kwaajiri yangu😜
 
Back
Top Bottom