uliwahi subiria safari kwa hamu af inakuja kuhairshwa mwshn enzi za utoto?ebu twambie ilikuwaj?

uliwahi subiria safari kwa hamu af inakuja kuhairshwa mwshn enzi za utoto?ebu twambie ilikuwaj?

enock yusto

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2014
Posts
377
Reaction score
341
Nakumbka mm wakati nipo darasa la nne alikuja mama mkubwa toka nairobi alinambia ukiwa wa kwanza tunaenda wote nairobi,mungu xaidia nkawa wa kwanza kweli darasani kwetu nkamkumbusha ahadi yake akaxema sawa hamna shida,nkaanza maandalizi ya xafari apo wiki moja kabla nkapanga nguo na kila kitu changu apo mbwembwe kibao kwa marafiki zangu kwamba naenda nairobi kwanza nlikuwa nina hamu ya kupanda ndege pil kuvuka boda,siku ya siku ambayo ndo siku yenyewe kuondoka nakumbka siku hiyo nililala mapema ili niwah kuamka,ila cha kushangaza nlipokuja kuamka nlikuta tayr mamkubwa kaondka!asee sitosahau niliumia sana marafk zangu walincheka na kuntania vibaya kwa fedheha,,,je kwako ilikuwaje?
 
Mimi ilikuwa tofauti kidogo na yako.

Nyumbani tulikuwa ni wakulima na pia tulikuwa tunafanya biashara ya kuuza karanga ambazo tunakusanya vijijini jirani na kwetu, tunakoboa halafu tunapeleka mkoani kuuza. Umbali kutoka kijiji chetu hadi mkoani ni 90 barabara ya vumbi halafu mbaya. Mabasi yalikuwa yanapita kijijini kwetu saa 11:30 za asubuhi yakiwa yametoka wilayani kama 11 km hivi.

Furaha yetu watoto ilikuwa ni kuwasindikiza madingi na kisha kuona gari (basi) linavyokuja kutokea mbali zile jinsi taa zinavyowaka basi ilikuwa burudani tupu, mizigo inavyopandishwa kwenye carrier ya basi na kisha gari kuondoka, basi tunajisikia raha mustarehe. Ili ufaidi yote haya inabidi uamke mapema kati ya saa tisa usiku ili pukurushani zote za kufikisha mzigo stendi uzishuhudie na kushiriki pia. Ha ajabu ilikuwa ni kwamba kulikuwa na mabasi matatu route hiyo moja linapita saa 11:30 asb, kisha linakuja la 12 na mwisho kabisa saa 1 kasoro. Lkn kutokana na kutakiwa kuwahi shule inabidi uwahi kuyaona yale ya saa mawili ya mwanzo ili ukajiandae kwenda shule ukawahadithie wenzio jinsi ulivyo 'mjanja'.

Siku moja nilikuwa nimepania kweli kweli, lakini usingizi haukuniruhusu nikajikuta nimeamka saa 12:30 hivi huku nasikia watoto wengine wa majirani ndio wanarudi kumsindikiza mzee wangu ambaye alisafiri asubuhi hiyo. Iliuma sana hadi leo nakumbuka.
 
Back
Top Bottom