Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Bila shaka kufanikiwa kwa mtu katika maisha inategemea mambo mengi sana na jambo mojawapo muhimu ni aina ya familia anayotoka.
Kwa watu wanaozaliwa katika familia tajiri "silver spoon" zenye kipato kizuri kutokufanikiwa ni wao waamue wenyewe kuharibu ila kwa wale wanaotoka katika familia maskini zenye kipato cha chini cha kuganga njaa tu maisha yasogee, zisizo na ardhi au mtaji, zisizo na elimu au koneksheni za maana njia ya mafanikio huwa ni jasho na damu, kama ni mchezo wa mpira tungesema wanaoanza maisha wakiwa nyuma 0-2 ,0-3 wakati wenzao wa familia bora wakiwa wanaongoza 2-0 na familia za kawaida 0-0
Uliwezaje kufanikiwa ikiwa umetokea familia masikini huku ukiwasadia baba, mama, kaka, dada, wajomba, shangazi, wapwa n.k wanaokutegema na kuhitaji msaada wako kuweza kujikimu? Mbinu gani ulitumia?