gimmy's
Povu la nini sasa?...hahahaha hata namna ulivyo ni attack inaonesha kabisa unahaki ya kutofata cheti chako kwa sababu hakina sifa ya wewe kuajiriwa!
Nilitegemea ungeona mantiki katika andishi langu na wewe kujenga hoja na sio mapovu!
Kama nilichosema si cha kweli si ungenijibu kwa hoja tu kuliko kunishambualia ambaye hata hunijui kwamba nimejiajiri au nimeajiriwa!?
Ukweli unauma. Ila lazima tuuseme. Kama umesoma na ukafaulu daraja la juu na ajira kugonga mezani kwako uliikataa ajira kwamba unakiherehere cha kujiajiri?
Labda umesomea mikozi ambayo inakusukuma kufanya kazi ambazo kamwe huzipendi na ulisoma kozi hiyo pasi kuitaka.
Hebu niambie nipe mfano aliyesoma na kupata kazi yenye mshara mnono sema TPA, SUMATRA, au TRA akakataa na kuenda kujiajiri kufuga kuku na kulima matikiti Kigamboni?
Usiwe na jazba jombaa, upo huko kwa sababu umekosa kuajiriwa katika mahali ulipokuwa unapataka!