Uliwezaje kumwongoza kijana balehe kimalezi kwenye umri wa upumbavu (foolish age)?

Braza Kede

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2012
Posts
3,840
Reaction score
6,844
Uliwezaje kumwongoza kijana balehe kimalezi kwenye umri wa upumbavu (foolish age)?

Umri una changamoto sana huu maana kijana ameanza kuutambua ulimwengu na mema yake.

Kipindi hiki kiburi kinakuwa kwenye ubora wake

Kama ni mkaka basi atajiona tayari kawa mbaba

Kama ni mdada basi atajiona tayari kawa mama

Kama ni mchepukaji utamjua kipindi hiki

Uliwezaje kudhibiti tabia za kijana katika umri huu?

Je ulifanikiwa au ilikuwa ni kama unampigia mbuzi gitaa ukitegemea atacheza?

Screenshot_20250111-234738_Instagram Lite.jpg
 
View attachment 3202343
Kwakweli hiki kipindi kigumu sana,
Nilikuwa na baadhi ya wadogo zangu wanapitia umri huo.. nilikuwa nawachapa sana makofi.. kuna mmoja ujeuri ulimtawala maana baadhi ya ndugu wakawa wanampa kichwa eti wanamuogopa... ila nilikaa nae nikamweleza kwamba "kwakuwa umekaza shingo na kuchagua njia ya upetevu basi nitakuwa nakuangalia tu, lakini omba Mungu ufanikiwe katika maisha yako, maana mambo yakikuendea kombo sijui utasema nini nikuelewe.. baada ya maneno hayo nikaachana nae,,, baad ya muda sijui kilimkuta nini akabadilika mwenyewe akawa kijana mzuri kabisa
 
Ni tofaiti kwa kila mmoja, kuna jirani watoto wake wanayo kali sana, wakike lazima waondoke nyumban kwa kugombana. Baadaaae ndo wanarudi, mi inawachanganya sana, wameanza wamama, sasa ni enzi za watoto wao.
 
Uliwezaje kumwongoza kijana balehe kimalezi kwenye umri wa upumbavu (foolish age)?

Umri una changamoto sana huu maana kijana ameanza kuutambua ulimwengu na mema yake.

Kipindi hiki kiburi kinakuwa kwenye ubora wake

Kama ni mkaka basi atajiona tayari kawa mbaba

Kama ni mdada basi atajiona tayari kawa mama

Kama ni mchepukaji utamjua kipindi hiki

Uliwezaje kudhibiti tabia za kijana katika umri huu?

Je ulifanikiwa au ilikuwa ni kama unampigia mbuzi gitaa ukitegemea atacheza?

View attachment 3202343
Ushauri wangu ungekuwa ogopa hii kitu kama nyoka,soma kwanza kujiingiza huku kuna gharama,tafuta helaaa,Mengine yawakubwa hayawafai watoto.Huyo ni kama Mama yako uwe na adabu.
 
Unaambiwa tumbo ndio hupumua makalio hutumika spika tu🤣🙌🥶
 
Nakumbuka enzi zangu nilikua mjeuriii yaani mtu haniambii kitu si nyumbani si shuleni, suspension kama zote 🙌🏻 baba angu alipambana sana, nashukuru kipindi kilipita salama,

Ushauri wangu kwa wazazi wa sasa anza kumshape mtoto kuanzia umri wa miaka 6, mpe kazi za nyumbani ajue kufagia, kumop, kuosha vyombo na kufua nguo nyepesi kama chupi na vest,

Akifika balehe mfanye awe busy sana, siku hizi kuna viwanja vya michezo tele akitoka shule mpeleke akacheze mchezo aupendao mfano pale Gymkhana mlipie awe anaenda au ule uwanja wa JK karibu na mnazi mmoja, kuna swimming classes, academies mbali mbali n.k lengo ni kumfanya mtoto awe busy asiwaze ujinga,

Simu/Computer unaweza usimpe na kama ukimpa basi control kila kitu, block apps zote za kijinga, hata youtube muwekee ya watoto, connect simu yake na yako ili kufatilia nyendo zake zote,

Zungumza na mwanao mfanye ajue dunia ni uwanja mpana sana kuna watu makatili wapo kwa ajili ya kuharibu watoto, mueleze kuhusu madhara ya mimba za utotoni mpe na mifano mbalimbali, mfanye awe huru na nyie akiwa na jambo lolote akimbilie kwa wazazi wake,

Mzoeshe kwenda Library na mnunulie vitabu vingi, kuna maarifa makubwa sana yanapatikana kwenye vitabu, tunarudi kule kule haya mambo mzoeshe tangu umri mdogo sio usubiri kishaanza kupata kibesi au kuota vichuchu hamtaelewana,

Pendelea kwenda nae kwenye kutoa misaada ya kijamii au kwenda nae vijijini hii itamfanya aheshimu maisha anayoishi ajue kua kuna wenzie kama yeye wanayatamani, itampa akili,

All in all, hayana fomula, ni kubahatisha tu.
 
umesema vizuri sana mkuu🙏🙏
 
Kwakweli hiki kipindi kigumu sana,
Nilikuwa na baadhi ya wadogo zangu wanapitia umri huo.. nilikuwa nawachapa sana makofi.. kuna mmoja ujeuri ulimtawala maana baadhi ya ndugu wakawa wanampa kichwa eti wanamuogopa... ila nilikaa nae nikamweleza kwamba "kwakuwa umekaza shingo na kuchagua njia ya upetevu basi nitakuwa nakuangalia tu, lakini omba Mungu ufanikiwe katika maisha yako, maana mambo yakikuendea kombo sijui utasema nini nikuelewe.. baada ya maneno hayo nikaachana nae,,, baad ya muda sijui kilimkuta nini akabadilika mwenyewe akawa kijana mzuri kabisa
kuna somo mujarabh kabisa hapo
 
Uliwezaje kumwongoza kijana balehe kimalezi kwenye umri wa upumbavu (foolish age)?

Umri una changamoto sana huu maana kijana ameanza kuutambua ulimwengu na mema yake.

Kipindi hiki kiburi kinakuwa kwenye ubora wake

Kama ni mkaka basi atajiona tayari kawa mbaba

Kama ni mdada basi atajiona tayari kawa mama

Kama ni mchepukaji utamjua kipindi hiki

Uliwezaje kudhibiti tabia za kijana katika umri huu?

Je ulifanikiwa au ilikuwa ni kama unampigia mbuzi gitaa ukitegemea atacheza?

View attachment 3202343
a6e67614bf7848aeb72172960088982d.jpg

Hiki kitabu ni kizuri sana mkuu Kwa malezi ya vijana hasa wanao barehe nk kitamjenga na kumwandaa Kwa ajiri ya utu uzima. Tafadhar nunua popote pale ulipo unatumiwa ni Hardcopy Kwa Tsh 10k nauli ya usafiri ni juu Yako. Hutajutia
13f87d816a604ac1b46784224531e424.jpg

Mimi nimekisoma hakika kina mambo mazuri sana hasa vijana walioko mashuleni/vyuoni....

Kipo Kwa lugha ya kiswahili

Unaweza uka ni pm au piga 0758585229 yupo Dodoma
 
Attachments

  • 5416ca26aa7b4e939e7e6c87c86447fd.jpg
    5416ca26aa7b4e939e7e6c87c86447fd.jpg
    74.3 KB · Views: 3
Balehe ilinikutia nipo form 3, nikaanza kulombana na beki3 wetu tena alikua amenizidi miaka 10+ alikua mdada wa kitanga halafu alikua fundi haswaaa.
Home nilikua navimba kmmk utafikiri mimi ndio baba mwenye nyumba, nilivyoanza kupiga na chuma nikapata kakikufua na kamkono basi kibri ndio kikazidi kuongezeka.
Aiseee kipindi hiki nahisi ndio kilikua kipindi chenye risk kubwa kuliko kipindi chochote kwenye maisha yangu.

Mbaya zaidi kampani yangu shuleni nilikua nimezungukwa na watoto wa waheshimiwa waliopinda, basi mbwa mimi pia nilikua najiona ni mtu mmoja muhimu flani hivi kwenye hii nchi.

Kikubwa kila nikikumbuka hicho kipindi hua namshukuru sana MUNGU kwa kunivusha salama bila ya kupata Ukimwi wala ajali za barabarani.
 
Balehe ilinikutia nipo form 2, nikaanza kulombana na beki3 wetu tena alikua amenizidi miaka 10+ alikua mdada wa kitanga halafu alikua fundi haswaaa.
Home nilikua navimba kmmk utafikiri mimi ndio baba mwenye nyumba, nilivyoanza kupiga na chuma nikapata kakikufua na kamkono basi kibri ndio kikazidi kuongezeka.
Aiseee kipindi hiki nahisi ndio kilikua kipindi chenye risk kubwa kuliko kipindi chochote kwenye maisha yangu.

Mbaya zaidi kampani yangu shuleni nilikua nimezungukwa na watoto wa waheshimiwa waliopinda, basi mbwa mimi pia nilikua najiona ni mtu mmoja muhimu flani hivi kwenye hii nchi.

Kikubwa nikikumbuka mpaka hii leo hua namshukuru sana MUNGU kwa kunivusha kipindi hicho bila ya kupata Ukimwi wala ajali za barabarani.
Natamani balehe yangu ningekuwa mtukutu kama wewe sema mimi mpole sana siwezi
 
Balehe ilinikutia nipo form 3, nikaanza kulombana na beki3 wetu tena alikua amenizidi miaka 10+ alikua mdada wa kitanga halafu alikua fundi haswaaa.
Home nilikua navimba kmmk utafikiri mimi ndio baba mwenye nyumba, nilivyoanza kupiga na chuma nikapata kakikufua na kamkono basi kibri ndio kikazidi kuongezeka.
Aiseee kipindi hiki nahisi ndio kilikua kipindi chenye risk kubwa kuliko kipindi chochote kwenye maisha yangu.

Mbaya zaidi kampani yangu shuleni nilikua nimezungukwa na watoto wa waheshimiwa waliopinda, basi mbwa mimi pia nilikua najiona ni mtu mmoja muhimu flani hivi kwenye hii nchi.

Kikubwa nikikumbuka mpaka hii leo hua namshukuru sana MUNGU kwa kunivusha salama bila ya kupata Ukimwi wala ajali za barabarani.
Kweli wewe mbwa ulinusurika maana kuzungukwa na watoto wa waheshimiwa ukajiona na wewe ni mheshimiwa
 
Balehe ilinikutia nipo form 3, nikaanza kulombana na beki3 wetu tena alikua amenizidi miaka 10+ alikua mdada wa kitanga halafu alikua fundi haswaaa.
Home nilikua navimba kmmk utafikiri mimi ndio baba mwenye nyumba, nilivyoanza kupiga na chuma nikapata kakikufua na kamkono basi kibri ndio kikazidi kuongezeka.
Aiseee kipindi hiki nahisi ndio kilikua kipindi chenye risk kubwa kuliko kipindi chochote kwenye maisha yangu.

Mbaya zaidi kampani yangu shuleni nilikua nimezungukwa na watoto wa waheshimiwa waliopinda, basi mbwa mimi pia nilikua najiona ni mtu mmoja muhimu flani hivi kwenye hii nchi.

Kikubwa nikikumbuka mpaka hii leo hua namshukuru sana MUNGU kwa kunivusha salama bila ya kupata Ukimwi wala ajali za barabarani.
daah mambo yalikuwa mengi mwamba ushukuru ulimaliza salama foolish age yako😆
 
Tunawategemea sana jamani mtupe abc zenu na mliowaona mkawasadia..yani kumbe kuna miaka tunafika tunaanza kuwaza tabia zetu za nyuma wakizipata wtt itakuwaje....
 
Mfanye rafiki, kisha muulize kuhusu ndoto zake, akikueleza mwambie upo tayari kumsupport kwa hali na mali kuhakikisha ndoto zake zinatimia. Mwambie ili ndoto zake zitimie, ni lazima ajiepusha na tamaa, makundi mabaya na nk..

Mwambie, safari ya kutimiza ndoto ina vikwazo vingi, hivo asisite kukushirikisha kila apatapo changamo ya aina yoyote.

Mtoe mara moja moja kila upatapo nafasi, mkumbushe juu ya ndoto zake, mwambie vile ulivyo na shauku ya kuona ndoto zake zinatimia na utakavyokua proud. Hii itamjengea kujiamini na kumfanya muda mwingi autumie kuumiza kichwa juu ya ndoto zake, jambo ambalo litampa wepesi wa kupambana na mihemko ya ujana bila yeye kujua.
 
Back
Top Bottom