Uliwezaje kununua gari yako ya kwanza?

Uliwezaje kununua gari yako ya kwanza?

feyzal

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2016
Posts
7,683
Reaction score
15,128
Wakuu habari ya hapa jukwaani.

Binafsi sina gari ila natamani sana kua na gari, mwaka 2017-2018 nilijaribu kufanya biashara ndogo ndogo na kuweka pesa ili angalau ninunue hata gari used ilipofika 2.3 M nikaangukia pua.

Mwaka 2020 nimeanza kujipanga upya ila sijajua mbinu ninazopaswa kutumia ili nimiliki gari. Kwa ninyi mliofanikiwa kununua magari naomba nielezwe mliwezajewezaje yaani je mlikopa bank, mliweka kwenye kibubu au ulitumia mbinu ipi kujichanga mpaka ukamiliki gari yako mwenyewe hata kama ni used.

Kipato changu kwa mwezi ni 500-700k japo nategemea kuongezeka 2021 kwa kua tayari nina vibiashara vidogo viwili.

Naomba mbinu wazee.

Nawasilisha.
 
Nilianza kufanya tafiti kati ya kununua Japan na Bongo wapi nitasave. Jibu likaja Bongo ila sio showroom.

Nikachuja gari zikabaki 5, IST, Runx/Allex, Passo au Raum.

Nikafanya Mchakato fasta CRDB wa 5 yrs (ungese sana kukopa muda mrefu, 3yrs ni idea nzuri).

Nikapata Mzungu flani anauza Runx 9M nikamuibukia bila fundi wala nn hapo najua tu kuendesha kdg. Akanipa A/C kesho nikuwekea mpunga nafuata gari na payin slip game over.

Sijawah kujuta.
 
Mkuu changia gari yako ya mkopo jinsi ulivyoipata itatusaidia sisi wenye shida na kumiliki mchuma
Naweka kambi,acha nione waliokopa kama mm[emoji318].
Huu uzi hauwahusu waliopewa zawadi sendoff na waliogawiwa na baba zao.
 
Shukrani Ndugu RROND ila mkopo kiukweli ..hapo lazima nikaze mkanda
Angalia kipato chako halafu weka lengo. Ila Kwa kipato cha 700k nafikiri mkopo utafanikisha lengo lako haraka.
 
Kwa watumish wa umma una save kias Fulani then unakopa kuongezea unapata gari used japan.suv ya kuanzia 13mil.
 
Nilianza kujaza kibubu. Kila mwezi laki 4. Baadae nikapanda hadi laki 5 kwa mwezi. Nili save kwa kama mwaka na nusu. Nikazama mtandaoni, baada ya kuona bajeti hairuhusu kununua ya hapa yard.

Nikapata ndinga kwa 3.3mil hadi kuifikisha Tanzania. Wakati huo $1 = Tsh 1730. Ushuru nikalipa 4.3mil. Tarehe 19/12 imefikisha miaka 6 tangu ifike. Ninaendelea kukamua nayo.
 
Hongera mkuu..pesa umesema uliweka kwenye kibubu? Au ulikua unamaanisha bank?

Nilianza kujaza kibubu. Kila mwezi laki 4. Baadae nikapanda hadi laki 5 kwa mwezi. Nili save kwa kama mwaka na nusu. Nikazama mtandaoni, baada ya kuona bajeti hairuhusu kununua ya hapa yard. Nikapata ndinga kwa 3.3mil hadi kuifikisha Tz. Wakati huo $1 = Tsh 1730. Ushuru nikalipa 4.3mil. Tarehe 19/12 imefikisha miaka 6 tangu ifike. Ninaendelea kukamua nayo.
 
Back
Top Bottom