Aisee huu uzi huu.
Mimi nilijichanga ikafika pesa ya kutosha kuagiza. Nikaagiza kibishi nikabaki sina hata mia.
Wakati gari imepakiwa melini nikaanza kujichanga pesa ya ushuru na port charges. Mungu si Athuman ndinga imefika nikawa nimepungukiwa kama milioni 3, nikachukua kwa washkaji zangu.
Kujichanga namaanisha mshahara na harakati nyingine nyingine za mtaani.
Ila nyie kuraise pesa 15+ ni kitu kigumu sana na inahitaji nidhamu na sacrifice ya hali ya juu sana, nilikua natamani sana nikachukue mkopo ila bahati mbaya sikua eligible sp nikakomaa.