Uliyeiba dera la dada huyu lirudishe kabla hayajakukuta makubwa

Uliyeiba dera la dada huyu lirudishe kabla hayajakukuta makubwa

Muda mchache uliopita nikiwa nimetulia zangu mahali nikasikia dada mmoja analalamika kuwa dera lake ambalo alilinunua kwa mkopo wiki chache zilizopita limeibwa wakati alipokuwa amelianika. Na zaidi dada huyo alikuwa analalamika kuwa hata mkopo wenyewe hajamaliza kulipa lakini tayari dera limeibwa.

Kwa hiyo kutokana na maumivu hayo nikamsikia akisema kuwa simu yake ikishajaa chaji tu, atampigia mtaalamu, ili mtendee manuva huyo mwizi wa dera lake. Kwa hiyo kwa kuwa mimi sipendi mtu apigwe kasumba kisa tu dera nimeamua kutoa taarifa kwa uma kuwa kama unajijua leo umeanua dera ambalo sio lako iwe kwa makusudi au bahati mbaya, lirudishe kwa mwenyewe kabla simu yake haijajaa chaji.

Ukichelewa simu ikapigwa kwa mtaalamu, my dear sister/brother, umekwisha. Dera litakutoa roho, Usijesema sikukuambia
Aliyeliiba kama sio Magonjwa Mtambuka basi ni miongoni mwa timu yao ya mapambio
 
Dela la mkopooh, litasafiri na roho ya mtu, uwiiiiiiiuuih
 
Back
Top Bottom