Uliza lolote kuhusu mgogoro ndani ya DRC hasa mapigano kati ya M23 na FARDC

Wewe upo dunia gani. Hapa GOMA sasa ni shangwe tupu watu wanashangilia ushindi. Unazungumzi crashes muda huu, na nani? Makenga kakimbilia RWANDA na BISIMWA katoa tamko. Nilikueleza awali kuwa safari hii ndiyo mwisho wa M23.

 
Wakumbuka shuka wakati kumekucha.

 

Mkuu you are trying to minimize your chagrin for the war losses by dis information.
Lete ushahidi, as we say in Bongo ..Hakatwi Mtu Hapa......
 
Kama ni hivyo basi hakika jamani tuungane pamoja kuwapongeza JWTZ.

 
Flash hider nipe habari,bila shaka unazo za ukweli
 
Unajua vita ni tool moja wapo ya kumaliza mgogoro huu. Kama nilivyozungumza awali, matatizo ya DRC ni makubwa na yanahitaji combination ya tools. Kubwa ni political na ikishindikana ni Vita. Unajua kama ingekuwa issue ni vita tu, basi kusingekuwa na Kampala Talks. Baada ya kuona hawa jamaa wanatumia Kampala Talks kama delaying tactics, ndipo matumizi ya nguvu za kijeshi yakafanyika. Sasa nasikia mazungumzo yanaendelea na pia DRC waliandaa kitu wanakiita STABILITY DIALOGUE (Check spelling) kujadiliana namna ya kumaliza tataizo hili. Rais Sasso Ngwesso ndiyo alikuwa mpatanishi na wamekubaliana mambo kadhaa ya kufanyika ili kuleta ustawi na amani ya kudumu katika DRC. MUNGU AWASAIDIE wafikie hapo walipojipangia.

ahsante kwa ufafanuzi wako mzuri mkuu

swal langu ni kwa hali ilivyo sasa,unaona vita ndo suluhisho la huu mgogoro?
 
Ukweli ni kuwa M23 hawapo tena DRC. Walikimbia baada ya kipigo kikali cha jana jioni hadi usiku. Serikali na raisi wa M23 ametoa matamko ya kuelezea hali hiyo. Muda huu hapa GOMA ni shangwe tupu baada ya matangazo hayo.

Flash hider nipe habari,bila shaka unazo za ukweli
 
Shwari kabisa na jamaa mjini ni shangwe tupu. Bodaboda honi mji mzima. Leo kuna mwananziki anaitwa WAZEKWA nasikia atatumbuiza usiku wa leo hapa GOMA kusheherekea ushindi.

Sasa mkuu nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu sana hili sakata la mapigano kati ya M23 na na majeshi ya serikari ya Congo, jana niliskia kwamba hawa M23 hawajaondoka Congo na badala yake wamesogezwa tu na sehemu walipokuwa awali, na habari zisizo rasmi niliskia kwamba wanakwenda porini kujipanga upya kwa ajili ya mashambulizi zaid, sasa mkuu FLASH HIDER unaweza kuongelea lolote kuhusiana na hili ?. Je, lina ukweli wowote ?
 
Bwana Flash Hider nakufuatilia kwa makini sana,hiyo nikawaida ya wakongomani wanasheherekea hata wakipigwa,vita bado haijaisha simuda murefu nitakupatia habari za front.

labda kama mtaanza vita nyingine ya kuwaua waganda na wahutu huko rwanda na si ndani ya mipaka ya DRC tena, tumewakata mikia.
 
Idhaa Ya Kiswahili

Matukio ya Kisiasa
M23 wasalimu amri, serikali ya Conyo yadai ushindi


Waasi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamesema wamesalimu amri baada ya kukabiliwa na mashambulizi makali na jeshi la serikali linalosaidiwa na Umoja wa Mataifa ili kuwaondoa katika eneo mashariki mwa nchi hiyo
Kundi hilo la waasi limesema katika taarifa yake kuwa "limeamua kuanzia leo kumaliza uasi wake" na badala yake litatimiza malengo yake "kupitia njia za kisiasa pekee". Hatua hiyo inamaliza uasi ambao umedumu miezi 18 na kuliharibu eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa raslimali na maliasili, lililokuwa kitovu cha mojawapo ya migogoro mibaya zaidi barani Afrika katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.
Awali, serikali mjini Kinshasa ilidai "ushindi kamili" dhidi ya M23 baada ya kuyakomboa maeneo mawili ya milima yaliyokuwa yametwaliwa na wapiganaji hao.
Lambert Mende, waziri wa mawasiliano na msemaji wa serikali, amesema "wapiganaji wa mwisho wa M23 wameondoka katika ngome zao", akiongeza kuwa sasa "waasi hao wamekimbilia Rwanda."
Naye Luteni Kanali Olivier Amuli, msemaji wa jeshi katika eneo la Kivu ya Kaskazini ambaye alikuwa katika eneo la mapigano amesema "tumemaliza kazi". Amuli ameongeza kuwa kabla ya kutoroka, waasi hao walichoma moto na kuziangamiza kabisa silaha zao, vifaa na magari waliyokuwa wamepora wakati wakiudhibiti mji wa Goma.
Jeshi la Congo lilisaidiwa na MONUSCO
Jeshi la Congo lilianzisha mapingano makubwa dhidi ya waasi mnamo tarehe 25 Oktoba, na kwa haraka sana likaweza kuzikomboa ngome zao hadi pale waasi mwishoni mwa wiki iliyopita walipoelekea hadi maeneo matatu ya juu ya milima takribani kilomita 80 kaskazini mwa mji mkuu wa eneo hilo, Goma, na karibu na mpaka wa Rwanda.
Waasi hao waliozidiwa nguvu walisalimu amri, lakini jeshi likaendelea na mashambulizi yao, na kutwaa mojawapo ya eneo moja la juu yam lima Jumatatu.
Jeshi Maalum la Umoja wa Mataifa nchini Kongo (MONUSCO), ambalo limekuwa likiwasaidia wanajeshi wa Kongo kwa kufanya uchunguzi wa angani, ujasusi na mipango, lilijiunga katika uwanja wa mapambano Jumatatu usiku baada ya kupata idhini ya kuziripua ngome zilizosalia za waasi. Chanzo cha habari kutoka Kikosi hicho cha MONUSCO kimesema "wataendelea kuvurumisha mabomu na kufyatua risasi hadi kila kitu kitakapodhibitiwa."
Safisha safisha yaendelea
Operesheni za safisha safisha bado zinaendelea, ili kuhakikisha kwamba hamna mpiganaji yeyote wa M23 aliye na silaha mkononi katika maeneo yote ya wilaya ya Rutshuru, walikokuwa wakiendesha harakati zao. Siku ya Jumapili, kiongozi wa M23, Bertrand Bisimwa, alitangaza kuweka chini silaha ili kutoa nafasi ya kuanzishwa tena mazungumzo. Lakini mapigano yalionekana tu kuongezeka, hata baada ya ombi hilo la kiongozi wa M23, licha ya taarifa iliyotolewa mapema Jumatatu na wajumbe kutoka Umoja wa Ulaya, Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa iliyosema kuwa "wana wasiwasi kuhusu machafuko yaliyoanzishwa upya" ambayo yalifuatia amri hiyo ya kusitisha mapingano.
Kwa miongo mingi, eneo la Kivu ya Kaskazini na Kusini katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limekuwa kitovu cha mzozo kwa sababu linazingirwa na mipaka ya Rwanda, Uganda, Burundi na Tanzania, pamoja na madini yanayopatikana kwa wingi katika milima ya eneo hilo.
Mwandishi: Bruce Amani/John Kanyunyu/AFP
Mhariri: Mohammed Khelef
 
Kama ni hivyo basi hakika jamani tuungane pamoja kuwapongeza JWTZ.

siri ya mafanikio haya ni historia tukufu ya ukombozi ya jeshi hili shupafu kusini mwa jangwa la sahara. Kinyume na ilivyokuwa kwa majeshi ya kinafiki na uvamizi kama rwanda, malawi na afrika kusini ya makaburu
 
PK kwa sasa atakua anaumwa tumbo,yule mwakilishi wa ITV hapo Goma ataleta taarifa zaidi toka Bunagana
 
Polini walikodai wamekimbilia ni hapo Tshanzu na Runyoni. Eneo hili linatajwa kuna lina misitu mikubwa na kuna milima na si rahisi kulifikia. Pia mbuga ya wanyama ya Virunga inapita eneo hilo. Pia eneo hilo lipo jirani na mpaka wa Rwanda na Uganda. Ilionekana ni vigumu kwa FARDC kulifikia. Hata hivyo FARDC na UN (JWTZ) walilizunguka eneo hilo na kushambulia kwa helikopta na mizinga. M23 Wakakosa pa kukimbilia na wakajikuta wakilazimika kuingia Uganda na wengine Rwanda. Lakini pia maeneo yote yaliyokuwa yanakaliwa na M23 kwa sasa yanakaliwa na UN. Bila shaka huu sasa ni mwisho wa M23.

 
Bila shaka wataleta coverage nzima. Leo huku ni sherehe, kazi zimafungwa.

PK kwa sasa atakua anaumwa tumbo,yule mwakilishi wa ITV hapo Goma ataleta taarifa zaidi toka Bunagana
 
this was SUNDAY if only its true.....and today is quite another day....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…