Uliza lolote kuhusu mgogoro ndani ya DRC hasa mapigano kati ya M23 na FARDC

hivi hujaona historia ambayo kaitoa kuhusu kiini cha mgogoro au mnataka mjaze thread bure??.

Twende taratibu, hakuna haja ya kufuka moshi na povu jingi kama tumegombana. Mleta thread hakuweka hiyo historia tangu mwanzo, bali amekuja kuileza baadaye sana. Huo ndio ulikuwa msingi wa hoja yangu ili wachangiaji wawe na uelewa wa kile kinachoendelea huko DRC.
 
.
Nakutaka radhi mkuu, ingawaje lengo langu ilikuwa ni kufikisha ujumbe kwa wahusika waongeze umakini katika utoaji habari wa masuala haya. Tusije tumia mbinu za saadam.

Hata hivyo nimeona uzalendo wako, nakupongeza kwa kazi nzuri.

Niombe radhi mkuu hapo kwenye jina ni peche sio Pache, pamoja sana.
 
Kaka ulivyo utamaduni wa Kitanzania, TUMESAMEHEANA na mimi nakumba radhi ya maandishi mabaya ya jina lako.

Karibu Goma

 
Tupo pamoja kaka

mkuu, ninasikia ya kwamba kutokana na vita hii nchi za Rwanda na Congo DRC hazina mahusiano mazuri kiasi ya kwamba DRC haina ofisi zake za ubalozi nchini Rwanda na vile vile Rwanda haina ofisi zake za ubalozi DRC. je ni kweli?
 
Mleta mada ubarikiwe sana. Huu uzi umekuwa ni wa manufaa makubwa sana kwetu. :amen:
 
nini kirefu cha m23?nani anafadhiri na mbinu zipi zaweza tumika kukata connection yao ya kumudu vita? hasa hapi goma kuna makabila mangapi?
jana nilimuona repota wa itv yupo frontline je wa jwtz anareport nini kama hawatujuzi na hata youtube hawaweki vitu kama vile live
 

ingekuwa vyema baada ya vita tuanze mchakato wa kufanya nao shirikisho la kisiasa kwa ajili ya kuwalinda.
 
Mada nzuri sana ,nimesoma mstari kwa mstari ,ila nikiongezea bila ya ushahidi ,Majeshi ya Tanzania yalimsaidia Kabila kabla ya hawa,M23kuibuka ,pale ulipotaja Zimbabwe na wengine ,bado Wajeshi waTz walikuwa mstari wa mbele ,kwani kila walipokatisha majeshi basi walikuwa wanazungumza kiswahili tena kiswahili swafi cha Kitanzania kwa maana huna haja ya kuuliza ni majeshi wa wapi.

Naamini hata WaKenya watatuhitaji kwenda kuisafisha Somalia.
 
Je ni kwel kwamba wapiganaji wa m23 wanapigana bila kuvaa kijeshi namaanisha wanavaa kiraia.? Km ni ivo usalama wenu km raia ukoje? Na je kuna kipind huwa mnaongea na askar wa tanzania huko mtaan
 

Uvivu wako tu wakutokushishughulisham, hiyo Historia ipo POST number 14 na alichofanya kwako kw akuw ani Mvivu ame-COPY na KU-Paste kwa jaili yako.
 
FLASH HIDER naweza kusema umejaribu na kupa 50%,kitu ambacho sikukubaliana na wewe nijinsi unavyo iweka tz juu sana katika hii vita,hajaongea kuhusu angola wao ndio wako mbele katika mapambano dhidi ya m23,kingine nimekua na wasiwasi na location yako kwani rwandair hajawahi kutua goma,kingine m23 haita isha kwani hivi wamebadilisha tactic sasa wameanza golira warfare ndio maana wamehamia virunga mountains,na itakua vita ndefu sana,nakushukuru umejaribu kuwaelimisha wabongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…