Uliza swali lolote kuhusu lishe ya mwanadamu

Naweza kupunguza uzito bila kufanya mazoezi?
Ndio inawezekana.
Na nisiathiri mfumo wa ulaji?
Hapo ndio penye mtihani, ni lazima kudhibiti lishe yako.

Kula vyakula vyenye afya, punguza kiasi cha chakula unachokula, na dhibiti mfumo wako wa ulaji.

Pia muda wa chakula hasa cha jioni/usiku, Hiki chakula yapasswa kiliwe mapema zaidi angalau masaa mawili kabla ya ule muda wako wa kulala.
 
Kuna vile vijamaa unakuta kanakula sana, hakafanyi zoezi na wala hata hakanenepi...

Wengine sasa unaweza kuwa unakula mlo mmoja tu ila kukonda SAHAU..!!!

shida ni nn hapa?
 
Kula sana au kula kidogo si kigezo cha mtu kunenepa au kutokunenepa, ingawa ulaji hovyo (yaani vyakula visivyo na lishe) unachangia sana kuongezeka kwa unene.

Chukulia huu mfano watu wawili:
- wanaokula mlo sawa kwa wakati sawa, na
- wanafanya kazi iliyo sawa,
Baada ya muda mmoja anaweza kunenepa na mwingine asinenepe, sababu za kibayolojia( Metabolism) au tabia zao ni tofauti, wahenga husema huyu kalizika japo anashindia kipande cha Muhogo angalia anavyo nenepa, hapa inajitokeza sababu nyingine ya kisaikolojia
Wengine sasa unaweza kuwa unakula mlo mmoja tu ila kukonda SAHAU..!!!
 
Kuna vile vijamaa unakuta kanakula sana, hakafanyi zoezi na wala hata hakanenepi...

Wengine sasa unaweza kuwa unakula mlo mmoja tu ila kukonda SAHAU..!!!

shida ni nn hapa?

Unene unategemea:-
1. Unakula nini?
2. Afya yako kwa ujumla
3. Mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
4. Shughuli unazofanya
5. Afya ya akili/Msongo wa mawazo
 
Naomba nijue vyakula vyenye lishe ni kama vipi
 
Naweza kupunguza uzito bila kufanya mazoezi? Na nisiathiri mfumo wa ulaji?

Mkuu unene ni matokeo ya uhifadhi wa chakula kilichmeng'enywa na kufyonzwa kuingia mwilini.

Nikimaanisha kwamba unapokula chakula kuna kingine kinatumika kwenye shughuli za kawaida afanyazo mwanadamu kuanzia kutembea, kuongea, kufikiri hapa kile chakula ulicho kula kinabadilishwa na kuwa nguvu. Sasa ukiona unanenepa maana yake chakula kimebadilishwa kimekua mafuta na kuhifadhiwa ndio maana unaongezeka.

Kwa maneno mengine naweza sema unachokula ni kingi kinatumika kidogo kingine kinabdilihshwa kuwa mafuta ndo utakuta unanenepo.

Sasa ukitaka upungue maana yake lazima upunguze kile chakula kilichohifadhiwa ndani ya mwili.Na kufanya hivyo ni lazima mwili utengenezewe shughuli za kutumia ndio maana unashauriwa kufanya mazoezi.

Kwa sababu ukisema upunguze kula tu utapunguza uingizwaji wa chakula tu lakini kile kilichokufanya unenepe kipo pale pale.Ni kama store iliyojaa na kile siku lazima uweke vitu sasa ukitaka store isijae maana inabidi upunguze vitu ambavyo uihitaji.

Ushauri kwanza punguza kula vyakula vyenye sukari au mafuta mengi maana ukiendelea kula hivi utazidi kuweka chakula zaidi, pili buni namna ya kufanya mazoezi na zoezi linalokata mafuta ni kukimbia.

Anza kidogo kidogo tafuta uwanja wa mpira kimbia kutoka goli moja kwenda goli la pili hata mara sita kwa week moja then baada ya hapa ongeza round kidogo kidogo kadri pumzi yako inavokuruhusu huku vyakula visivyo na mafuta miezi mitatu utaona mabadiliko.
 
Naomba lishe 5 zenye nguvu ya kupambana na saratani mbalimbali
Mkuu hakuna chakula kinachoweza kupambana na saratani na wala mtu asije kukudanganya hata siku moja kwamba kuna hiko kitu kwasababu zifuatazo.
Saratani ni matokeo ya moja kati seli kupata hitilafu katika DNA ambazo hizi hupatikana ndani ya kitovu cha seli. Sasa inapotokea hivi hizi seli zinaanza kuwa na tabia tofauti na kusababisha cancer. Sasa mtu unapokula chakula cha aina yoyote iwe ugali,mboga za majani vinamengenywa mfano vyakula vya protein labda samaki ikimengenywa inabdilishwa inakua molecule ya amino acid kwa hiyo kinachoingia ndani ya mwili ni hiyo amino acid sasa inasafirshwa kupelekwa sehemu inapohitajika na kila aina chakula kinavunjwa na kinanyonywa kama molecule.

Sasa tuseme mtu amepata cancer lishe inayotokana na chakula inapofika huko kwenye seli zilizoathiriwa zinatumiwa kwa matumizi ya kawaida na wala hakiwezi kuzuia seli zilizoharibika wala kuzipa kinga ya aina yoyote ile.Kwahiyo kitatumiwa na hiyo seli ili ikue na pia kumbuka kwamba ili chakula kama kifike kwenye seli maana ni mwili umeruhusu imefika kule kwa hiyo kinachoingia mwilini kama chakula kinatumika kama chakula. Hakuna lishe ya kupambana na saratani
 
Hapo nimeelewa. Kwa maneno mengine Cancer ni sawa uasi wa baadhi ya seli kutaka kuchukua mamlaka za umiliki wa mwili kwa namna tofauti na mwili ulivyo zoea.

Vipi hatuwezi kuzitumia seli ambazo hazijaasi kushambulia zile zilizo asi?
 
Hapo bado hatujafikia huko ila kuna wanasyansi wanjaribu kutumia dna ya hizi seli za cancer kutengeneza protein ambazo zatasaidia kuepuka utengenezwaji wa seli zenye uasi
 
Back
Top Bottom