Ulokole

Ulokole

Dogoli kinyamkela

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2024
Posts
618
Reaction score
1,440
Unageuka kichaa ama chizi anayejua anavaa nguo nzuri
Na kwenda kwenye jengo fulani kukutana na wenzake.

YAANI paka anaweza pita nyumbani kwako,kisha akakutizama wewe
Kwa kukukodolea macho tu,

Nawewe kwa upumbavu wako unatangaza mfungo hapo nyumbani siku 7,
Yaani unasumbua watoto kwenye lishe kisa ujinga wa HOFU,na WOGA wako,

MJUSI anaweza kuanguka na kufia karibu na vyombo,utawaalika wajinga wenzio mnaotishwa na hofu ya mauti,ukidhani ni watumishi waje kupiga kelele hapo ndani,,,,ukidhani ni ""NI MAOMBI YA VITA""
Pasipo kua na ufahamu huyo ni kiumbe tu alikuwa anajitafutia insects

UTAMKUTA mwanamke kishaolewa na anawatoto tayari,Ghafla analipukwa na transformer ndani ya ubongo,anakimbia familia yake

Anasema BWANA ameniambia huyo sio mume wangu,amesema atanipa wa kufanana naye toka nyumbani mwake.

Mpuuzi mkubwa wewe,

Siku hio inarekebishwa unajikuta umegaragazwa na kijiji cha watu mnaoitana wapendwa....!!
Heshimu mume yako,hio haikuwa bahati mbaya
Kusudi linatengenezwa na

Kutaka kwako,kunia kwako pamoja na kutenda kwako...
Kwani kabla hujaolewa naye hukuwa na hivi vitu vitatu.?
Kama hukua navyo basi ulikuwa roboti linaloendeshwa.!

MLOKOLE
Unakopa hurejeshi unasema bwana atafungua madirisha
Madirisha gani wewe? Nenda kafagie hata mabanda ya ng'ombe ulipe deni la watu.
Huo muda unaoshinda hapo kanisani huzalishi kitu.

UKIWA maskini
Unawehuka unaona kila kitu kiko against nawewe.
Hakuna watu waongo kama maskini
Hakuna watu wanaongoza kumlaumu MUNGU kama maskini
Hakuna watu wanaongoza kusengenyana kama wanaoitana wapendwa.
Mikutano,na shemasi wanafanyia majumbani kwako leo,kesho habari utazikuta za jinsi unavyoishi.
Maskini ni mwizi.
Maskini ni dhalimu.
Maskini ni mchawi kabisa ndani ya fikra zake.

TOFAUTI
Ya maskini na kukosa hela
Masikini ni mtu mwenye tatizo katika mfumo wa fikira na akili
Kukosa hela ni kitendo cha wakati fulani tu.

HITIMISHO
Ukiamua kuwa mlokole anza kwanza kujenga msingi mzuri
Ndani ya fikra zako
Ili baadae usije ukaona kila mtu ni adui yako,
 
Back
Top Bottom