Inawezekana ila kama utaweza kukumbuka muda ambao ulikutana na mwenza wako.. Yaani sio mara ya mwisho kukutana nae, ila mara zote mlizokutana uwe una kumbuka tarehe...
Ukiwa na hizo kumbukumbu unaweza kujua kama ujauzito ni wako au la!
Ultrasound inaweza kuzalisha picha ya kiumbe kilichopo katika mfuko wa uzazi na daktari anaweza kukuambia kina mda gani, yaani kama ni miezi miwili au mitatu na kadhalika!!!
Sasa kama wewe ukiona mahesabu ya daktari na yako hayaendani basi hapo jua tayari kuna walakini na huo ujauzito..