Umaarufu (sifa) chanzo cha kifo cha Dj Arafat

Umaarufu (sifa) chanzo cha kifo cha Dj Arafat

Ng'wanapagi

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2013
Posts
9,116
Reaction score
8,652
Jana ilikuwa siku ngumu sana kwa tasnia ya mziki Afrika hususani nchini Congo na Ivory Cost. Hii ni baada ya mwanamziki na DJ maarufu sana kijana DJ Arafat kuaga dunia kwa ajali mbaya ya pikipiki akiwa anaendesha (anaichezea) kwenye barabara kuu za mjini Ivory Cost.

Katika video iliyonaswa na CCTV DJ Arafat anaonekana akiiandaa pikipiki yake huku wafuasi wake wakimshangilia akiwa hana hata kofia ngumu maarufu helmet na vifaa vingine ambavyo huwa naona waendesha pikipiki kubwa za mashindano wakivaa. Baadae anaonekana akiendesha kwa madaha (akiendesha kwa kutumia tairi moja yaani mbele imeinuka!! Baadae anaweka miguu juu ya sehemu ya kukalia na mwisho anaonekana akiiparamia gari na kufa palepale.

Kwa haraka utaona kabisa umaarufu wake hakujali sheria za barabarani wala polisi wa usalama barabarani. Huyu ndie alikuwa DJ special wa wanamziki wa Congo waendapo kupiga show Ivory Cost ukizingatia wanaongea lugha moja (French) na kafanya colabo za kutosha.

R.I.P bro

FB_IMG_1565672929730.jpeg
FB_IMG_1565672912174.jpeg
FB_IMG_1565672969388.jpeg
FB_IMG_1565673027283.jpeg
 
Amekufa kizembe, ila Mungu ndiye ajuaye mtu atakufa kwa namna gani pengine angekwepa hilo angeangukiwa nyumba
R.I.P
 
Yuko mmoja hapa mtaani kwangu,simuombei mabaya ila dah jamaa anajiamini sana,hizo show kama alizokuwa nafanya huyo marehemu hapo juu huwa anazifanya sana...
 
Yuko mmoja hapa mtaani kwangu,simuombei mabaya ila dah jamaa anajiamini sana,hizo show kama alizokuwa nafanya huyo marehemu hapo juu huwa anazifanya sana...
Mtaje tu ajirekebishe tunajifunza kupitia makosa
 
Back
Top Bottom