Umaarufu wa Original Comedy, B12 na Lil Ommy umeshuka sana

Umaarufu wa Original Comedy, B12 na Lil Ommy umeshuka sana

Broadcast

Member
Joined
Jun 19, 2022
Posts
76
Reaction score
285
Aiseee Maisha yanabadilika fasta sana..

Leo hii huwezi amini Original comedy wanafanya show halafu hakuna anayeshtuka. Hakuna anayejishughulisha nao

Vipi kuhusu B12 Wa Clouds FM, aisee kijana wangu amepotea kabisaaaa nahisi alitengenezwa awe wa Clouds FM kule alifit sana

Lil Ommy ameshuka aisee sio wa Times FM kabisaa kuna hatua nyingi amerudi nyuma
 
Original comedy akina mtanga au[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Sio kweli Data zinakataa, yaani Lil Ommy wa times fm awe maarufu kuliko wa wasafi!! acha kuchekesha , times fm ni radio ya uchochoroni, kuhusu B12 inawezekana maana clouds ilikuwa na fan base kubwa kuliko E fm
 
Vijana wa mjengoni naona mnapata tabu,hayo ni maisha ya mtu na maamuzi ya mtu binafsi kutokana na maslahi yake.
 
B12 amekuwa kwenye industry kwa muda Sasa, naamini sio chini ya miaka 20, kutegemea umaarufu wake ubaki vile vile ni kujitekenya mwenyewe na kucheka.
Hata hao original comedy night hivyo hivyo pia.

Ni muhimu kuelewa nyakati zinabadilika Ndugu. Binafsi sikumbuki hata radio nimesikiliza mara ya mwisho lini. Sana Sana nasikiliza redio kwenye daladala.
 
Mkuu na wewe ubadilike sasa uache kupanda daladala.

Ofcoz lil ommy anawaumiza kichwa sana media za bongo kaishika nchi vipindi vya mchana number ndio zinazungumza hivyo
 
Mkuu na wewe ubadilike sasa uache kupanda daladala.

Ofcoz lil ommy anawaumiza kichwa sana media za bongo kaishika nchi vipindi vya mchana number ndio zinazungumza hivyo
Gari binafsi Sina, uwezo wa taxi Sina, baiskeli Wala pikipik sina , Sasa nisipopanda daladala nipande punda!?
 
Kuhusu Orijino Komedi ni nyakati tu ndio zimebadirika. Sasa hivi comedy zimekua nyingi sana mitandaoni, mtu anaangalia muda wowote. Tofauti na zamani hamna sehemu ambayo ungeweza kuangalia comedy tofauti na kipindi cha Tv.

Kuhusu B12, kapotea. Yani hapo hamna cha nini wala nini. Move ya kuhama clouds ni kama alikua anajizamisha baharini. XXL + comb yake na Mchomvu, vilikua sio vitu vya kuviacha. Labda kama kuna sababu nyingine.

Lil Ommy sijawai kufatilia kazi zake. Kwaio sijui hata trend yake imeendaje
 
Back
Top Bottom