pingli-nywee
JF-Expert Member
- Sep 16, 2015
- 11,923
- 13,350
Timu ya Kenya ya mpira wa wavu, Malkia Strikers, ambao ndio mabingwa wa Afrika walifuzu hivi majuzi kuiwakilisha Afrika kule Tokyo, 2020 Olympics. Waliibuka mabingwa na point 11 kwenye mchuano wa kufuzu. Tena walishinda mechi zao zote, 3-0 dhidi ya Nigeria, 3-2 Cameroon, 3-0 Botswana na 3-1 dhidi ya Misri. Timu ya raga7s pia, Kenya Lionesses, ilifuzu mwezi uliopita kuiwakilisha Afrika kule Tokyo, 2020 Olympics.
Wao pia walishinda kwenye mechi zao zote hadi fainali, 36-0 dhidi ya Senegal, 49-0 Botswana, 36-0 Ghana na 26-5 dhidi ya Zimbabwe, S.A ikawashinda 15-14. Harambee Starlets(soka) nao wakaibuka mabingwa wa CECAFA baada ya kufunga mabao 24 bila kufungwa bao hata moja! Siku chache kabla ya hiyo walikuwa wamefika fainali kwenye mchuano wa kufuzu kufika kule Tokyo. Ila Zimbabwe wakaibuka washindi 1-0. Hongera zao, bendera ya Kenya izidi kupepea kotekote. [emoji1139]