Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Baada ya kupata Uhuru wa Tanganyika, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwatangazia watanganyika kwamba nchi yao ilikuwa na maadui watatu ambao ni Umaskini, maradhi na ujinga. Ili kuyaondoa hayo mambo matatu, pia Mwalimu akasema kuwa tunahitaji watu, Ardhi, siasa safi na Uongozi bora.
Tangu wakati huo mpaka mwaka 1977 TANU ilipoungana na ASP na kuunda CCM, nchi hii haijawahi kuongozwa na chama kingine cha siasa.
Ukiona Dokta Ulimboka anang'olewa kucha jua ni kwa sababu CCM iko madarakani.
Ukiona wanafunzi wa shule za msingi wanasoma zaidi ya mia darasani ni kwa sababu CCM iko madarakani.
Ukiona watu wanatekwa, wanateswa na wengine hata kuuawa na watu "wasiojulikana" jua ni kwa sababu CCM iko Madarakani.
Ukiona mpaka leo watu wanakunywa maji machafu ya kwenye madimbwi kwa kushirikiana na Ng'ombe, elewa hivyo ndivyo CCM inavyotaka waishi.
CCM ndiyo ilikuwa madarakani wakati mabilioni ya Pesa yanachotwa toka Benki Kuu na kwingineko.