OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 426
- 685
Sina shaka na ufahamu wa umasikini alionao Rais juu ya uchumi CV yake inaonesha amesoma Economic Development. Naamini alikuwa anawachezea shere wahariri kwa kuwachanganya kidogo, bahati mbaya uelewa juu ya umasikini waliokuwa nao wahariri ulikuwa na walakini hivyo wakashindwa kumrudishia hoja Rais. Hata hivyo nimeona haja ya kutia neno kwenye tafsiri ya Umasikini aliyotumia ili kuweka hoja kuwa hakuna maskini Tanzania.
Rais ametumia fedha kama kipimo cha umasikini ambacho kimsingi kimeshakosolewa na wachumi tangu miaka ya 80. Hali hii ilileta namna tofauti za kutafsiri umasikini na maendeleo ili kuweza kufit kwa context ya kila nchi. Kwa sababu hii nitazungumzia umasikini kwa kuzungumzia maendeleo ili tuwe na maana bora ya umasikini na tujue kama kweli maskini wapo au la.
Kwanza niseme hoja yangu haitakuwa kuhusu Tanzania bali watanzania. Tanzania ina rasilimali nyingi ila watu wake ndio balaa.
Baada ya fedha kukosolewa kama kipimo cha umasikini, umasikini ulianza kuangaliwa kwa dimensions nyingi ikiwemo, afya, elimu na kipato, ambapo hapa tunakutana na Human Development Index (HDI) iliyoanza kutumiwa na UNDP tangu mwaka 2010. Kipimo hiki ni sehemu ndogo ya matokeo ya watu kama kina Amrtya Sen ambao walileta Capabilities Approach inapokuja kwenye suala la maendeleo.
Capabilities Approach ya Sen inaangalia zaidi command aliyonayo mtu dhidi ya mazingira yake. The real Freedoms of the people. Yaani kama maji yako mtoni, je mtu huyu anaweza kiasi gani ku-command maji yamfuate ndani kwake, badala ya maji kum-command yeye ayafuate mtoni? Kadhalika na kwenye vitu vingine.
Sasa tuzungumzie tu suala la maji, mbali na kwamba mamlaka za maji zinaunganishia watu maji(hata kama hayatoki) ni wangapi wanaweza kumudu gharama za kuwekewa maji majumbani mwao, kwa mujibu wa sensa kaya zenye mabomba ni chini ya 53%. Aidha suala la afya, linaangaliwa kwa uwezo wa mtu kuishi muda mrefu, kutokana na uwezo wa kudhibiti maradhi nk. Je, tunafuatilia kwa ukaribu vifo vya magonjwa kama maleria, kipindupindu nk, wanaokufa kwa maradhi hayo ni kina nani na kwa nini?
Suala la Wahadzabe
Rais ametaja wahadzabe wanakula matunda ambayo kama ukiyapa bei inaweza kuwa wanatumia fedha nyingi sana ila wao wanayapata bure. Hili jambo ni kweli kabisa. Hata hivyo, kwa kuangalia "command" suala la mwanadamu kuanza "Animal keeping" lilikuwa ni suala la maendeleo na kupunguza umasikini badala ya kila siku kwenda porini. Yaani ukifananisha mmasai ambaye anafuga na muhadzabe, muhadzabe hana amali yeyote. Sasa hatuwezi kusema sio masikini wakati kimsingi hawana mali na wanaishi kwa bahati nasibu, maana kwenda porini haimaanishi kuwa utapata mnyama kila siku. Hapa zinahitajika tafiti kuangalia wastani wa umri ambao wahadzabe wanaishi kwa kufananisha na makabila mengine, na mtaona kwanini kukosa command kwa wahadzabe kunawapunguzia muda wao wa kuishi. Umeshawahi kumuona mzee wa kihadzabe? Ni suala la kujisifu?
Point kubwa ni kwamba kuna tofauti ya mtu kuwa survivor na mtu kuishi. Wahdzabe ni ma-survivors hawaishi. Yaani ni sawa na kuusifu muhindi ulioota sehemu yenye nyasi nyingi, ukasema hakuna haja ya kufikiria rutuba.
Je, tutatumia njia tofauti zaid ya Capabilities approach kujua ni kwa namna gani watu wetu ni masikini? Au tutabaki kwenye traditional measures ambazo hazitumiki kivile kuzunguzia maendeleo?