mangiTz
JF-Expert Member
- Jul 28, 2019
- 1,820
- 3,062
Habari za muda huu wana jF
Katika tukio la kusikitisha na la majonzi ,huko mkoani Tanga , mwanamke mmoja amefariki wakati wa kujifungua kwa kukosa huduma ya matibabu ambayo alitakiwa kulipa TSH 150,000 kwa ajili ya operation kwa mujibu wa taarifa ya chanzo cha habari kilivyoeleza.
Inaelezwa kuwa mariam Zahoro alikuwa anajifungua lakini katika harakati ikashindikana ikatakiwa afanyiwe upasuaji lakini alishindwa kulipa gharama hiyo hivyo kupelekea kupoteza maisha.
Nimesema umaskini ni wa kupiga vita kubwa kwasababu kifo cha huyu mama kinahuzunisha , inawezekana huenda siku yake ilikuwa bado haijafika ila jitihada zimekoma kwa ufukara , just imagine kuna watu wanapoteza maisha kwa kukosa 150,000 , lakini je hivi hospital hawana huduma za dharura kumsaidia mtu kama huyu mnajua kabisa hali yake mbaya? Ndio akaachwa atajua mwenyewe? Umasikini unakosesha vitu vingi sana katika familia yako pambana hili lisikukute likimbie.
Ukitaka kujua kubwa na uwezo wako kifedha ni vizuri angalia hili tukio , sasa imebaki watu watasimuliana tu. Hivi hakutokea hata Msamaria mmoja kunusuru hili.
Nimesikitishwa pia na mama mzazi , anasema mwanae(marehemu) anamwambia basi kama ndio hivi mimi nakufa akanishika mkono huyo mama (mzazi wa. Marehemu) anasema haya mwanangu nitafanyaje sina uwezo" kauli ambayo sijaifurahia
Wizara ya Afya Tanzania
Source: ITV