Umasikini ni Kikwazo cha Ukuaji Demokrasia Afrika

Umasikini ni Kikwazo cha Ukuaji Demokrasia Afrika

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
3,211
Reaction score
3,611
Kuna mtazamo duniani kuwa wasio na kazi ya kipato ndiyo hutengeneza hadhira kwa wanasiasa majukwaani na pia hufanyika ama wateja au abiria wa difenda na karandinga.

Umaskini wa kipato unakwaza ukuaji wa demokrasia barani Afrika:

1. Chaguzi za Afrika zimeghubikwa na rushwa hatarishi kwa mustakabali mbovu wa ukuaji wa demokrasia Afrika.

2. Watu kupenda posho ili wahudhurie majumuiko ya harakati za kisiasa vinginevyo hawaoni umuhimu wa harakati hizo kulinganisha na shughuli zao mbalimbali za kuwaingizia vipato.

3. Vyama vya siasa visivyokuwa na ruzuku vinakabiliana na changamoto za ukuaji kisiasa na kuathiri mchakato wa demokrasia.

4. Ombaomba ya fadhila inayofanywa na vyama huvibebesha madeni makubwa na pengine kukata tamaa kwa wafadhili, kufuatia kutoona tija ya fadhila zao kwa vyama vya siasa.

5. Mzigo wa gharama kubwa unaosababishwa na mlundikano wa kesi za kisiasa zikiwemo za chaguzi.

Ukuaji wa uchumi huchagiza ukuaji wa demokrasia kinyume na hilo umaskini ni kikwazo cha ukuaji demokrasia Afrika.
 
Back
Top Bottom