Umasikini ule ulitutesa sana, Isijirudie tena...


Mkuu, this is 2019?? Technology has gone so far, Stop being stranded in the past. Dunia haiko hivyo tena.
 
Mkuu, this is 2019?? Technology has gone so far, Stop being stranded in the past. Dunia haiko hivyo tena.
Sijaelewa unataka kumaanisha nini. Kila nyakati huwa na teknolojia ya wakati wake nayo huwa ni ya hali ya juu kwa wakati husika.

Hii mada inahusiana nini na maendeleo ya Teknolojia?
 
IMF Wakikutaa hakuna mmagharibi atakayekukopesha,atakayenunua treasury bills zako,atakayekuja kufanya uwekezaji wa maana kwako,atakayekupa msaada,kama walikuwa wanakudai na muda wa kulipa deni umefika hautapa huruma ya debt restructuring.
Sijuaji kwani hawa IMF wakiikataa nchi yoyotre kinachofuata ni ukame .
Mfano angalia Zimbabwa na Nchi nyingine ziliingia kwenye mtego huu
 
IMF na WB ni pande mbili za shilingi moja,AFDB inapata pesa zake nyingi kutoka huko huko kwa hao 'mabeberu' nchi za Scandinavian no wananchama na washirika thabiti wa WB na IMF,hivyo ulichokiandika hapa ni ugoro mtupu.
Kuhadiwa kupatiwa hiyo mikopo/misaada ni jambo moja,kupewa baada ya kutimiza vigezo na masharti ni jambo lenginie,rejea ahadi ya ule mkopo wa USD 300M kwa ajili ya elimu na wanafunzi wanaopata mimba kama umeshapatikana mpaka sasa
 
Brain-app kuna watu hawajui kwamba hata hiyo China tunayoiona kama ndiyo mkopeshaji wetu salama na yenyewe inakopa huko kwa mabwana wakubwa hao WB/IMF.
 
Uzi wa wakongwe tu huu
 
Kiwango kikubwa cha raia wetu hawana elimu ya zaidi ya darasa la saba,waliofanikiwa kufika elimu ya juu wana uelewa finyu sana kwenye eneo la elimu ya uraia,basics za uchumi na global affairs ambayo ni mambo ya msingi sana kwa mtu yeyote aliyefika angalau elimu ya juu pasipo kujali taaluma yake.
Brain-app kuna watu hawajui kwamba hata hiyo China tunayoiona kama ndiyo mkopeshaji wetu salama na yenyewe inakopa huko kwa mabwana wakubwa hao WB/IMF.
 
Mku si unajua hakuna anayekubali kufanya yasiyo na faida kwake.
Tukumbuke kila kinachozalishwa Afrika kama soko liko kwao bei hatupangi sisi Wafrika
 
Ni kweli, hakuna mtu mwenye akili anayekubali kufanya biashara au mahusiano yasio na faida kwake, muhimu ni kuangalia na sisi tunanufaikaje na kama kuna makosa yalifanyika yarekebishwe kwa utaratibu sahihi pasipo ugomvi usio na ulazima.
Katika uchumi wa soko huria duniani kote sio mzalishaji pekee anayepanga bei ya bidhaa,ni nguvu za soko na ushindani ndizo zinaamua bei ya bidhaa zako. Dhahabu inazilishwa Tanzania,Ghana, South Africa,Russia,Mali,USA n.k zote zinakutana katika soko mwenye bei ya chini na bora ndiyo inanunuliwa,vivyo hivyo kwa kahawa kutoka Tz, Uganda,Brazil, Vietnam n.k,vivyo kwa maghari kutoka US, Japan na Ulaya kuja kwetu
Mku si unajua hakuna anayekubali kufanya yasiyo na faida kwake.
Tukumbuke kila kinachozalishwa Afrika kama soko liko kwao bei hatupangi sisi Wafrika
 
Watu hawali principle mzee, watu wanahitaji mahitaji muhimu!
Hayo mambo ya Nyerere kujifanya mwanafalsafa, mwenye misimamo, eti isiyoyumba ilitusaidia nini sisi wakati wa njaa kali?
Ni nani aliyekufa njaa Tanzania.
Kuna huna unaloliamini na kulisimamia maishani mwako, wewe ni binaadam; una tofauti gani na ng'ombe au nguruwe?
Nashangaa sana kwa uelewa wako ambao nimeuona hapa JF mara kwa mara, unaweka mawazo kama hayo hapo juu!
 
Huwa hatutaki kukubali udhaifu wetu huu. Sio wakati ule tu, bali hadi sasa. Kama taifa hili ndilo tatizo letu kubwa.
 
Ni nani aliyekufa njaa Tanzania.
Kuna huna unaloliamini na kulisimamia maishani mwako, wewe ni binaadam; una tofauti gani na ng'ombe au nguruwe?
Nashangaa sana kwa uelewa wako ambao nimeuona hapa JF mara kwa mara, unaweka mawazo kama hayo hapo juu!

Hata misimamo isiyo na maana nayo ni misimamo, lakini madhara yake ni makubwa sana
 
Acha bange za mchana wewe chokoo... Washamba wenzenu wameharibu uchumi kutokana na fikira pimbi, leo unazungumzia TL kwa lipi? Kweli watu wasipokuwa na elimu wanakuwa hawana faida kwa nchi
Mwambie sasa Tundu Lisu aache ujinga anaoufanya kama kweli unamaanisha na hutak turud huko.
A
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…