mkongongojo
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 245
- 156
Enzi zile mkibahatika kuwa na ndugu anafanya kazi ktk duka la RTC, familia yenu imeula; maana bidhaa chache zilizopatikana ziliuzwa kwa kujuana tu, hamna namna nyingine.
Hapo ulipoanzia ulanguzi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Enzi zile mkibahatika kuwa na ndugu anafanya kazi ktk duka la RTC, familia yenu imeula; maana bidhaa chache zilizopatikana ziliuzwa kwa kujuana tu, hamna namna nyingine.
SioKwahiyo wanakatwa shingapi kwa gharama za hiyo miamala???
Au ukiwa na tsh 1000 panama wewe ni taita??
IMF watolewe kabisa kwenye hili, maana hata uchumi ukikua huwa hawahusiki.
Nakumbuka zama zile za miaka ya 1983 hadi 1984, niko tunaishi mitaa ya Makutano Mabibo jijini Dar es salaam na Kadi yangu ya Rangi ya Kijani ikiwa na maelezo ya Kaya yetu ndani Mwake.
Mchana wa jua kali la Darisalama tukiwa tumekaa barabarani kusubiri gari la "Ugawaji" litaelekea mwelekeo upi na sisi tulifukuzie kwa nyuma. Hakuna aliyejua leo ni zamu ya duka gani kupelekewa chakula ama mahitaji mengine muhimu ili wakazi wa eneo letu waende wakanunue.
Shuleni wanafunzi wanavaa nguo zisizo na rangi maarufu kama "Maradufu" kutokana na viwanda vya kuzalisha nguo kukosa rangi za kuweka ili vitambaa hivyo viwe na rangi ya Bluu Maalum zama hizo kwa sare za shule za msingi.
Mitaani watu wanavuta sigara kwa "Puff" kwa hela ulizo nazo. Watu wanafua nguo zao kwa kutumia majani ya mpapai, sukari inakaangwa ili kutengeneza chai kwa kuwa hakuna majani ya chai na wenye majani ya chai wanaweza kutumia sukari guru badala ya sukari ya kawaida kama kiungio.
Unakwenda kwenye duka la ushirika kwa mfano kununua Sukari unalazimshwa kununua na kitu kingine kwa mfano Chujio la chai ama birika. Watu wa Darisalama tuliteseka sana na wanawake wengi walibakwa na watu waliojifanya wana bidhaa hizo "adimu" majumbani mwao..
Wakati ule Mgambo na wenyeviti wa maduka ya Ushirika walikuwa kama ni Miungu watu. Sisi kwetu kulikuwa na mgambo aliyetembea na wake za watu alivyopenda kisa yeye ana nafasi kubwa sana ya kupata vitu kwenye duka la Kaya la Mtaani kwetu.
Hayo yote yalisababishwa na Ugomvi wa Mwalimu JK Nyerere na wakubwa wa IMF na World Bank. Umaskini ule ulitutosha hatutaki hali ile ijirudie tena kwenye kizazi hiki.
CC: Mshana Jr Pascal Mayalla
Sijaelewa unataka kumaanisha nini. Kila nyakati huwa na teknolojia ya wakati wake nayo huwa ni ya hali ya juu kwa wakati husika.Mkuu, this is 2019?? Technology has gone so far, Stop being stranded in the past. Dunia haiko hivyo tena.
Sijuaji kwani hawa IMF wakiikataa nchi yoyotre kinachofuata ni ukame .
Mfano angalia Zimbabwa na Nchi nyingine ziliingia kwenye mtego huu
Kuna kitu kikubwa ambacho wengi hawajaona ktk kauli ya IMF (kama ikithibitishwa ni kweli wametoa hio kauli):
Miradi mingi ya Maendeleo inayotekelezwa na GoT inafadhiliwa/inakopeshwa na washirika wa maendlzeo kama WB, AFDB, JICA ama Scandnavian countries, na hilo hufanyika baada ya wao kuridhika na mapendekezo na mpango wa utekeleza wa GoT.
Ni muda mrefu sasa tangu IMF itoe mkopo/msaada wa aina yeyote ile kufadhili miradi ya Maendeleo ktk TZ. Hali ni tofauti kwa WB, AFDB, JICA ama Scandnavian countries ambao wako bega kwa bega na GoT na hata zikitokea tofauti hua zinamalizwa and life goes on bila kushinikizana kwa kutumia magazeti au waandishi wa habari wa Kenya.
Haingilii akilini kuona IMF ianatoa matamko yanayo pingana na washirika wengine ndani ya siku 2 tu tokea washirika hao (WB, AFDB, JICA) waingie makubaliana ya mikataba ya kukopesha TZ zaidi ya Tsh Trillion 2 za utelelezaji wa miradi ya maendeleo.
Eti IMF wanaita miradi hio kuwa haina maaana kwa Maendeleo ya TZ, swali la kujiuliza, je hivi washirika hao wengine wa maendeleo hawajaliona hilo wakati wanafanya due diligence kabla ya kukubali kutoa hizo fedha za miradi (i.e, BRT, SGR, Elimu, Steglers, Afya)?
Kwa hali ilivyo inawezekana kabisa:
Ikumbukwe kuwa IMF ni chombo amabacho kimekuwa kikutumiwa kuharibu uchumi wa nchi nyingi duniani kuanzia Latin Amerika (Brasil, Argentina) , Ulaya (Greece, etc), Asia na hata Afrika (Kama OP ulivyoeleza enzi za Mwl. Nyerere au hata Kenya miaka ya hivi karibuni). Huwa wanashinikiza nchi husika kufuata maelekezo yao kama vile kuuza viwanda vya ndani, kubinafsisha SOEs etc na baada ya hapo hali huwa inabadlika kuwa mbaya zaidi nya awali na huleta uasi na machafuko ya kijamii.
- Kuwa IMF wanafanya maksudi ili kutengeneza hali ya hofu na kuchafua investment climate ya TZ duniani ili wabia wetu wa maendleo na wawekezaji waogope kushirikiana na GoT. Then tuwapigie magoti wao waje na bail-outs kutuokoa at their own terms; ama
- kuwa kuna watu walioko ndani ya TZ na nje wanashirikiana kwa kupeleka habari hasi IMF ili kuishinikiza GoT ibadili misimamo yake kwenye mambo kama sera za madini, energy (umeme), etc, ili GoT ikubali kuweka sera za kunufaisha makampuni yao.
Cha muhimu ni kwa GoT kuhakikisha Kuwa haichukui mkopo wa aina yeyote toka IMF period. Kama tayari mikopo hio ilikuwepo toka zamani basi wendelee kuilipa lakini kamwe wasikuckue mikopo yao mipya.
Kwahiyo IMF walikuza uchumi wa tz!!!
Uzi wa wakongwe tu huuNakumbuka zama zile za miaka ya 1983 hadi 1984, niko tunaishi mitaa ya Makutano Mabibo jijini Dar es salaam na Kadi yangu ya Rangi ya Kijani ikiwa na maelezo ya Kaya yetu ndani Mwake.
Mchana wa jua kali la Darisalama tukiwa tumekaa barabarani kusubiri gari la "Ugawaji" litaelekea mwelekeo upi na sisi tulifukuzie kwa nyuma. Hakuna aliyejua leo ni zamu ya duka gani kupelekewa chakula ama mahitaji mengine muhimu ili wakazi wa eneo letu waende wakanunue.
Shuleni wanafunzi wanavaa nguo zisizo na rangi maarufu kama "Maradufu" kutokana na viwanda vya kuzalisha nguo kukosa rangi za kuweka ili vitambaa hivyo viwe na rangi ya Bluu Maalum zama hizo kwa sare za shule za msingi.
Mitaani watu wanavuta sigara kwa "Puff" kwa hela ulizo nazo. Watu wanafua nguo zao kwa kutumia majani ya mpapai, sukari inakaangwa ili kutengeneza chai kwa kuwa hakuna majani ya chai na wenye majani ya chai wanaweza kutumia sukari guru badala ya sukari ya kawaida kama kiungio.
Unakwenda kwenye duka la ushirika kwa mfano kununua Sukari unalazimshwa kununua na kitu kingine kwa mfano Chujio la chai ama birika. Watu wa Darisalama tuliteseka sana na wanawake wengi walibakwa na watu waliojifanya wana bidhaa hizo "adimu" majumbani mwao..
Wakati ule Mgambo na wenyeviti wa maduka ya Ushirika walikuwa kama ni Miungu watu. Sisi kwetu kulikuwa na mgambo aliyetembea na wake za watu alivyopenda kisa yeye ana nafasi kubwa sana ya kupata vitu kwenye duka la Kaya la Mtaani kwetu.
Hayo yote yalisababishwa na Ugomvi wa Mwalimu JK Nyerere na wakubwa wa IMF na World Bank. Umaskini ule ulitutosha hatutaki hali ile ijirudie tena kwenye kizazi hiki.
CC: Mshana Jr Pascal Mayalla
Brain-app kuna watu hawajui kwamba hata hiyo China tunayoiona kama ndiyo mkopeshaji wetu salama na yenyewe inakopa huko kwa mabwana wakubwa hao WB/IMF.
Sio kazi ya IMF kukuza uchumi wa nchi yako.Unaukuza wewe mwenyewe kwa kuzingatia kanuni za msingi za kiuchumi na kuondokana na sera mbaya zinazotatiza ukuaji.
Mku si unajua hakuna anayekubali kufanya yasiyo na faida kwake.IMF na WB ni pande mbili za shilingi moja,AFDB inapata pesa zake nyingi kutoka huko huko kwa hao 'mabeberu' nchi za Scandinavian no wananchama na washirika thabiti wa WB na IMF,hivyo ulichokiandika hapa ni ugoro mtupu.
Kuhadiwa kupatiwa hiyo mikopo/misaada ni jambo moja,kupewa baada ya kutimiza vigezo na masharti ni jambo lenginie,rejea ahadi ya ule mkopo wa USD 300M kwa ajili ya elimu na wanafunzi wanaopata mimba kama umeshapatikana mpaka sasa
Sasa habari hapa iwe mapungufu ya magu, sio IMF kukatazwa.
Bila shaka wewe ndiye huelewi,hata tumeanzia wapi.IMF kukatazwa nini?
Wewe huenda huelewei kinachozungumzwa hapa,huu mjadala ni kama umekuzidi kimo,bora ukae kimya.
Mku si unajua hakuna anayekubali kufanya yasiyo na faida kwake.
Tukumbuke kila kinachozalishwa Afrika kama soko liko kwao bei hatupangi sisi Wafrika
Ni nani aliyekufa njaa Tanzania.Watu hawali principle mzee, watu wanahitaji mahitaji muhimu!
Hayo mambo ya Nyerere kujifanya mwanafalsafa, mwenye misimamo, eti isiyoyumba ilitusaidia nini sisi wakati wa njaa kali?
Huwa hatutaki kukubali udhaifu wetu huu. Sio wakati ule tu, bali hadi sasa. Kama taifa hili ndilo tatizo letu kubwa.Lakini kilichochangia pia uchumi kuwa mbaya siyo IMF bali ni mis-management kwenye mashirika ya umma...uzalishaji ulikuwa wa ovyo kabisa kwenye mashirika ya umma ..wanyakazi wengi kwenye mashirika lakini hawazalishi...inefficiency ilikithiri kwenye mashirika na serikalini na kadhalika na kadhalika.
Ni nani aliyekufa njaa Tanzania.
Kuna huna unaloliamini na kulisimamia maishani mwako, wewe ni binaadam; una tofauti gani na ng'ombe au nguruwe?
Nashangaa sana kwa uelewa wako ambao nimeuona hapa JF mara kwa mara, unaweka mawazo kama hayo hapo juu!
AMwambie sasa Tundu Lisu aache ujinga anaoufanya kama kweli unamaanisha na hutak turud huko.